MARA

Contact +255717274387/+255759417639
info@kangetakilimo.co.tz

Description

Wadau walioshiriki katika mafunzo walielimishwa juu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu na vinyunyizi. Washiriki wa mafunzo walielekezwa kuhusu umuhimu wa kusoma vibandiko kwenye viwekeo vya viuatilifu ili kupata taarifa muhimu kuhusu kiuatilifu husika. Washiriki walielezwa kuwa kibandiko kinatoa taarifa zinazohusu jina la biashara, jina la sumu (Kiambato amarifu), ujazo wa kiuatilifu, aina ya mchanganyiko wa kiuatilifu, 

namba ya usajili inayothibitisha kiuatilifu kutumika Tanzania, kiwango kinachotakiwa kuchanganywa na maji, muda wa mwisho kutumika na maelezo ya huduma ya kwanza pindi mtumiaji anapodhurika. Pia washiriki walielekezwa aina na namna ya kuvaa vifaa kinga pale mtumiaji wa viuatilifu anapokuwa stoo ya viuatilifu, kabla ya kupima kiwango kinachotakiwa na kuchanganya na maji, unyunyiziaji shambani. Washiriki walielekezwa aina ya nozeli na matumizi yake.

Location

Mara

About Kangetakilimo

Is the Agricultural gateway to untapped Agricultural Resources and markets targeting poor small scale, medium scale and large scale farmers in Tanzania, in providing access to crucial Agricultural solutions and Technology Services, products and solutions. Kangetakilimo enables and empowers local Farmers by .... Read more

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.