Kilimo cha Bamia

Kilimo cha Bamia

Bamia ni zao la Jamii ya mbogamboga linalotambulika kitaalamu kama Abelmoschus esculentus (OKRA) lenye asili ya Afrika ya magharibi. Kwa sasa zao hili linalimwa katika nchi nyingi hasa sehemu za joto. Baadhi ya maeneo yanayolima zao la bamia kwa Tanzania ni pamoja na ukanda wote wa nchi ya Tanzania,Kutoka mita 0-1500 kutoka usawa wa bahar

i zaidi ya hapo unaweza kulima lakini halivumilii hali ya baridi kali.Pia bamia hufanya vizuri zaidi katika maeneo yenye udongo wenye unyevu wa kutosha na joto la wastani wa nyuzi joto 25 - 30 C.

 Mvua hadi  kiasi cha milimita 1000 cha mvua kwa mwaka.tu asili yake ni africa nchini Ethiopia ambapo kwa sasa linalimwa katika nchi  nyingi.bamia ni moja kati ya mazao ambayo yanafaida sana ndani ya mwili kama kusafisha utumbo mpana husaidia kulainisha choo huongeza uroto kwa wale wenye upungufu wa uroto kwenye maungio pia ina vitamin C ambayo husaidia kulainisha ngozi na macho kuona

 AINA ZA UDONGO

Kuna aina kuu tatu za udongo,

• Kichanga (Sand soil) –

una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.

• Tifutifu (Loam soil) –

 unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.

• Mfinyanzi (Clay soil) –

 unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.

 Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:

 

Ø Tindikali ya udongo

Ø Kiasi cha mboji

Ø Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium.

Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa. Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)

PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0)

.Ila bamia Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katikakipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

AINA YA UDONGO UNAOFAA KWA ZAO LABAMIA

BAMIA hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia halinaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya

MAANDALIZI YA SHAMBA LA BAMIA

Taarisha shamba lako mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi na masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.Magonjwa kama yale ya majani hayatatokea yatakuwa kidogo. Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu .Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na MIMEA kutastawi vizuri. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:

1.                 Jembe la mkono - wengi wanatumia

2.                 Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe

3.                 Power tillers

4.                 trekta

ZINGATIA

Tunashauliwa kupanda bamia katika matuta ili kusaidia mizizi kukua vizuri na udongo kuhifadhi maji. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.

AINA ZA BAMIA

Kuna aina za bamia zinazo patikana  kama vile

1. Clemson spineless.

Ain ya bamia hii inatabia ya kukua urefu wa mita 1 hadi 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu karibu sm 15. Huchukua siku 55 hadi 58 kuanza kuvuna.

2. Emerald green.

bamia hii ina tabia ya kukua hadi urefu wa m 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu wa sm 18 hadi 20. Huchukua siku 58 hadi 60 kuanza kuvuna.

3. White velvet.

 bamia hii inatabia ya kukua urefu wa m 1.5 hadi 1.8 na kuzaa bamia ndefu, nyembamba, zilizochongoka na zenye urefu wa sm 15 hadi 18.

 UWANDAAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani. Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za bamia zinazoweza kupandwa na kutoa mavuno bora kama vile Lady’s Finger, Quim Bombo, Asutem, Mkulima-Clemson Spineless, Labadi Dwarf.

UPANDAJI WA BAMIA

Mbegu za bamia mara nyingi husumbua kidogo kuota kama patakuwa  na hali ya baridi katika udongo.Hivyo ili ziote vizuri tunashauriwa kabla ya kuzipanda shambani ziloweke katika maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 au ziloweke kwa dakika 30 katika ethly alcohol and acetone,.

 panda mbegu zako katika mashimo uliyoyachimba katika udongo wenye unyevu kwa kina cha sentimeta 2 -3 katika nafasi ya sentimeta 60-90 kati ya mstari na msatari na sentimeta 25-50 Kati ya shina na shina  utahitajika katika kila shimo uweke mbolea kwa ajili ya ukuaji mzuri wa Bamia zako  

kutumia mbolea ya kuku au ng'ombe amabayo ni bora zaidi kwani ya kuku huisha kazi yake mapema zaidi katika udongo.Panda Mbegu mbili  kwa kila shimo na zikisha ota ngolea uache shina moja kwa kila shimo.kiasi cha kilo 1.5 - 2.5 hutosha kwa ekari moja ambapo wingi wa mbegu itategemea uwezo wa mbegu kuota na aina ya bamia.Kama mbegu zako uwezo wake wa kuota ni mdogo mbegu zitatumika nyingi na kama unapanda bamia fupi au bamia zenye mbegu kubwa  mbegu itatumika nyingi pia.Mbegu za bamia zinaweza kuchukua siku 8 - 10 kupanda hadi kuota.Pia bamia unaweza kupanda mbegu katika kitalu baadaye zikifikisha sentimeta 10-15 unazing'oa na kwenda kupanda shambani ila njia nzuri ni kupanda moja kwa moja shambani

PALIZI                                                                                                                                           

Katika kilimo cha bamia ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda.nashauri kwamba katika kilimo cha cha bamia shamba lipaliliwe mara 1-2, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono kwa kung’olea au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES). 

MFUMO WAUMWAGILIAJI

Hali ya unyevunyevu ni mdogo katika shamba itahitajika uwe unamwagilia shamba lako kila baada ya siku 10 au pungufu kulingana na hali ya unyevu katika shamba lako.Kiasi cha wastani wa milimita 350 za maji katika siku 10 zinahitajika kwa ukuaji wa bamia ili uweze kupata mavuno yaliyo bora na mengi.na kama umepanda mbegu katika kipindi cha ukame zimwagilie kila siku kuhakikisha udongo wako unakuwa na unyevu wa kutosha ili kuwezesha mbegu zako kuota.

MBOLEA

Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.

Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea

Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:

1. Mbolea za asili (organic fertilizers)

    2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)

Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile: 

     i. Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.

      ii.  Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.

     iii.  Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.

    iv.  Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.

      v.  Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.

Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)

Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

RATIBA YA MBOLEA KATIKA ZAO LA BAMIA

HATUA YA KWANZA

(Tunashauri Kapadia kwa Samadi kama ikiwepo)

NPK 15.9.20 +TE(yaramila winner) Gramu 10 kupanda bila kuweka samadi

Yara mila winner Gram 5 pamoja na samadi kwa shina / shina moja

Tenganisha kwa kuweka tabaka la udongo usio na mbolea kwa sentimita mbili kati ya mbengu na udongo uliyochanywa na mbolea

Epuka mbegu kugusana na mbolea inaweza kuungua na kushindwa kuota

HATUA YA PILI(A) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KATIKA UDONGO

NITROBAR (CAN)

Weka mbolea ya kukuzia ya nitrobar wiki tatu baada ya mche kuota  au mche wenye majani matatu(3)baada ya utokaji .

Weka mbolea ya ujazo wa kifuniko cha soda /kijiko kimoja kidogo cha chai sawa na gramu tano katika kila shina la mche mmoja

Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia  zingatia kuweka mbolea hii mapema kabla ya kutoa maua

HATUA YA PILI (B) KUWEKA MBOLEA  YA KUKUZIA  KUPITIA MAJANI(BUSTA) BAMIA

MULT-K AND SUPERGRO/NPK+TE foliar –pulizia mbolea hii kwa miche ikiwa na majani matatu hadi manne ya kuchipua

Changanya MULT-K maganda matatu ya kibiriti katika maji ya lita 20 puliza juu ya majani ya mche

Rudia tena baada ya siku kumi na nne (14) zingatia kutumia mbolea,

Mbolea hii ni mtiririko wa mbolea ya kukuzia sambamba na nitrobar izingatie kutumia kabla ya maua

HATUA YA TATU KUWEKA MBOLEA YA UZALISHAJI WA MATUNDA YA

Maua na matunda yatakapotunga wiki ya sita na nane weka tena npk 15.9.20+ TE(yaramila winner) gram 10 kwa shina (kijiko cha chakula)

Weka mbolea au  umbali wa nchi 6 mzunguko wa shina unaweza kuongeza gram 5 hadi 10 baada ya siku ya 21 kama kuna viashirio vya upungufu wa rutuba shambani kwa kuangalia ubora matunda na muonekano wa majani ya matikiti

WADUDU NA MAGONJWA YA BAMIA

1)WADUDU

A) Mdudu mafuta (aphids)
Hufyonza majimaji katika majani na bamia changa hivyo kusababisha bamia kutokuwa vizuri na bora.

   Kinga na tiba 

 Tumia dawa za wadudu kama vile ABAMECTIN, NIMEBECIDIN FARMER GULD, ACTARA,n.k

          B) MIilibagi (Mealy bug)
Ni wadudu wanaoganda katika majani,matawi na bamia wakifyonza maji maji ya mimea

Kuzuia na Kinga-Tumia dawa za wadudu kama vile selecron 720,Nimebecidin,multimectin,Dudu all,ninja nk n.k

c)Funza(Boll worm)
Hawa ni funza amabao hutoboa na kuharibu Bamia

Kinga na tiba 
Kwa maeneo yanayoshambuliwa sana na wadudu,Puliza dawa za wadudu mara tuu bamia ziwekapo ua na zikiwa ndogo,Puliza asubuhi sana au jioni sana ili kuwakwepa wadudu wachavushaji wasije kufa na dawa wakati unapuliza.Puliza dawa kama vile Nimebedicin,albamectin n.k kuua wadudu hawa

d) Funga funga(Leaf roller)
hufunga majani kwa kuyavilingisha na kukaa na kula majani hayo.

kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all n.k

e) Inzi weupe (whitefly)
Ni waenezaji wakubwa wa magonjwa ya virusi, wadudu hawa hufyonza majimaji katika majani ya mimea na hujificha sana chini ya majani wakati wa jua kali


kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all,actara, n.k

f) Vinundu katika Mizizi(Root –knot nematodes)
Ni wadudu wadogo kama minyoo midogo ambao hula katika mizizi midogo na kusababisha uvimbe na mimea kusinyaa.

kinga na tiba 
tumia dawa kama vile NIMEBECIDIN (kwa kiasi kikubwa Chini ya shina La mmea), DAZOMET (BASAMID),CARBOFURAN(FURADAN) kuua wadudu hawa.Hizi ni  dawa za ardhini.

2) MAGONJWA YA BAMIA
Bamia hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile;

a) Ubwiri unga (Powdery mildew)
Ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu).ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivu katika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani.

TIBA NA KINGA
Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza dawa za ukungu zenye salfa kama vile copper sulphate, na siku za upuliziaji itategemea muda wa kulima bamia masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.

b)Ugonjwa wa kujikunja na kudumaa majani (Leaf curl)
ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ni ugonjwa  ambao huambatana na kujikunja kwa majani machanga na kuwa magumu  na mmea kudumaa kukua

KUZUIA NA KINGA

 

-panda mbegu kinzani na ugonjwa huu,tumia madawa ya ukungu kama vile Copper sulphate, au puliza sulpha au copper  (BONIDE).Pia tumia dawa za wadudu kuua wadudu kama nzi weupe  ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu.

c) Ugonjwa wa manjano(Mosaic)
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi amabapo mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.KUMBUKA rangi ya njano ya majani inaweza kusababishwa pia na ukosefu wa nitrojeni katika mmea hasa kama maji yatakuwa mengi ardhini katka udongo

KUZIA NA KINGA

kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu.zui wadudu katika shamba lako kwani wanaweza kueneza ugonjwa huu shambani kwako.Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa  sigara/tumbakukatika shamba la bamia wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la bamia.Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya bamia.

10. JINSI YA KUVUNA BAMIA
Bamia huwa tayari kuanza kuvunwa mwezi 1 tangu kupandwa na huckukua siku 6 kuvunwa baada ya kuanguka.kama matunzo ni mazuri kila ua katika mabamia litatowa bamia.chuma vizuri bamia kutoka katika mbamia bila kuacha athari kubwa katika mche wa mbamia.

Hivyo kwa uvunaji mzuri unaweza kutumia mkasi mkali katika kukata vikonyo vya bamia.chuma bamia kubwa na ndogo ziache ziendelee kukua,ila inakubidi uwe mwangalifu ili bamia zisije kukomaa shambani kwani hukomaa kwa haraka zaidi na zilizokomaa hazina soko zuri na hazipendwi na walaji kwani huwa gumu na nyuzinyuzi nyingi.

Katika matunzo mazuri unaweza kuendelea kuchuma bamia kutoka katika mibamia kwa muda wa miezi miezi 2 na zaidi.

MAVUNO

wingi wa mavuno hutegemea matunzo na aina ya mbegu za bamia,muda wa upandaji na kukua-baridi ikiwa kali mavuno yake hupungua na mara za uchumaji wa bamia-kadri zinavyochumwa mara nyingi ndivyozinavyozidi kuzaa na zile zinazozachumwa kwa muda mrefu ndizo zenye manufaa kwa mkulima , japokuwa kwa wastani  bamia huvunwa kiasi cha tani 3 - 10 kwa ekari


11.UHIFADHI WA BAMI
Bamia ni kama mazao mengine ya mbogamboga haistahimili kukaa muda mrefu bila kuliwa na kadri inavyokaa muda mrefu baada ya kuvunwa ndipo hupoteza ubora wake.Kama kuna soko hakikisha unazivuna na kuzipeleka sokoni.

Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo

 

 

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.