KILIMO CHA MATIKITI MAJI

KILIMO CHA MATIKITI MAJI

Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.

Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi

Moja kati ya changamoto kwa wakulima wengi wa wa matikiti kutokufanikiwa kutokana  na mashambulizi ya nzi wa matunda aina Melon fly ambae husababisha hasara kwa kiwango cha 50% hadi 80 %ya matunda mengi kuaribika na kusababisha hasara kwa wakulima

Melon Fly (Bactrocera Cucurbitae)Nzi wa matunda ndio wadudu hatari namba moja dunia  kwa uwaribifu wa matunda Mzunguko wa maisha yake huanzia kwa jike kutanga mayai ndani matunda na mboga mboga kama melon, cucumber na tomato crops pia hushambulia flowers, stem, root tissue

kwa kutumia mwiba mkali mwishoni mwa tumbo lake uitwao msinzi akiwa na umri wa siku tano hadi wiki nane mayai huanguliwa ndani ya tunda na kuwa funza ambao hukua ndani ya tunda huku wakila nyama ya tunda au mboga na kusababisha tunda kuoza na kudondoka chini kisha funza kutoka ndani ya tunda na kujichimbia ardhini kiasi cha sentimita mbili hadi tano na kuwa buu matunda yaliyoshambuliwa kwa kila tunda moja linaweza kuwa na wastani wa funza 60 hadi 100 kwa kila tunda.Njia tunapendeka kuzibiti nzi wa matikiti aina ya bactocera ni kutumia njia za IPM kama kutumia mitego aina ya kangetakilimo fruitfly aina ya augmentorium,pia unaweza kutumia njia ya kuweka chombo chenye protini kuweza kukamata 

 

KILIMO CHA MATIKITI MAJI HATUA YA KWANZA

Hakisha nafasi kati mche na mche unaweka 1m kwa kupanda mbegu 2 au 60sm kwa kupanda mbegu 1.Pandia mbolea ya DAP(yaramila OTESHA) Gramu 10 kupanda bila kuweka samadi

Yara mila OTESHA Gram 5 pamoja na samadi kwa shina / shina moja tenganisha kwa kuweka tabaka la udongo usio na mbolea kwa sentimita mbili kati ya mbegu na udongo uliyochanywa na mbolea epuka mbegu kugusana na mbolea inaweza kuungua na kushindwa kuota kama utatumia samadi ya ng’ombe weka viganja vitabu vya mikono yako miwili zingatia matumizi ya samadi ya ngombe sio vizur kutumia kwenye mazao ya muda mfupi ili kuepuka minyoo.

HATUA YA PILI(A) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KATIKA UDONGO

 NPK YARA MILA WINNER UA NPK 17:17:17

 Weka mbolea ya kukuzia ya YARAMILA WINNER (NPK 17:17:17)wiki tatu baada ya mche kuota  au mche wenye majani matatu(3)baada ya utokaji .Weka mbolea ya ujazo wa kifuniko cha maji ya uhai /kijiko kimoja kidogo cha chai sawa na gramu tano katika kila shina la mche mmoja baada ya siku 10 utaweka mbolea tena  kwa ajili ya kukuzia.Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia  zingatia kuweka mbolea hii mapema kabla ya kutoa maua

 

HATUA YA PILI (B) KUWEKA MBOLEA  YA KUKUZIA  KUPITIA MAJANI(BUSTA)

 Tracel Bz/NPK+TE foliar aau mbolea yoyote ya maji au unga yenye ratio ya npk 21:21:21  –pulizia mbolea hii kwa miche ikiwa na majani matatu hadi manne ya kuchipua.Changanya Tracel BZ au ya Npk 19:19:19 maganda matatu ya kibiriti katika maji ya lita 15 hadi 20 puliza juu ya majani ya mche pamoja na udongo

Rudia tena baada ya siku kumi na nne (14) zingatia kutumia mbolea hii kabla ya maua kutoka.Mbolea hii ni mtiririko wa mbolea ya kukuzia sambamba na nitrobar(CAN) zingatie kutumia kabla ya maua

 

HATUA YA TATU KUWEKA MBOLEA YA UZALISHAJI WA MATUNDA YA MATIKITI

 Maua na matunda yatakapotunga wiki ya sita na nane weka mbolea ya nitrabor au mbolea ya can gram10 kwa kifuniko cha maji ya uhai kama umepanda miche miwili weka VIFUNIKO 2

 Weka mbolea au  umbali wa nchi 6 mzunguko wa shina unaweza kuongeza gram 5 hadi 10 baada ya siku ya 21 kama kuna viashirio vya upungufu wa rutuba shambani kwa kuangalia ubora matunda na muonekano wa majani ya matikiti


HATUA YA 4 KUWEKA MBOLEA YA UZALISHAJI WA MATUNDA YA MATIKITI

Baada ya matunda kutoka na kufikia kiasi cha kichwa cha mototo au ngumi utaweka mchanganyiko wa mbolea mbili NPK yaramila wina(npk 17:17:17) na Mbolea ya Nitrobar(can) kila baada ya siku 7 utakuwa unaweka hadi kuvuna kiwango cha gram 20 sawa na vizibo viwili vya maji ya kuchwa chupa ya maji ya uhai

 

JINSI YA KUPRUNI MATIKITI

Baada ya matunda yako kukua na kufikia kiwango cha kiganja cha mkono wako unatakiwa kufanya pruni ili kupata matunda makubwa na yenye ubora mzuri hakikisha unakuwa makini kwenye kufanya pruni hasa unatakiwa kupunguza matunda na kuacha matunda matatu kwa kila mche au mawili ila hakikisha kwanza umeweka mitego kwa ajili ya melonfly

 Shina  moja la mche wa matikiti hutoa matawi mengi kuanzia matatu na kuendelea hakikisha kwamba unapofanya pruni unatoa na matawi ambayo hayana matunda na yale yenye matunda  kuyakatia vikonyo ili yasiendee ili tunda liweze kunenepa vizur kwa ushaur zaidi tupigie

No2: KUZIDHIBITI APHIDS NA WADUDU WENGINE

 Baada ya utoajia majani mawili hadi matatu.tumia dawa yenye kiambata cha imidacropid nacypemethrin  kama farmerguard au rapid attack,attacan n.k kwa mchanganyiko wa pulizia mls 20 ml/20 l ya maji katika majani ya mimea na shina na kunyonywa na mmea Rudia tena baada ya siku 14 hadi 21

 

No3: KUDHIBITI  WADUDU WANAOCHORA MAJANI NA KUTOBA MATUNDA

 Tumia dawa za wadudu aina ya acetameprid +abermectin (Wadudu wanaochora) Pamoja na cypermethrin+profenofos (Wadudu wanaotafuna na kutoboa matikiti) acetameprid +abermectin vipimo 20-30ml/20l, cypermethrin+profenofos vipimo 40ml/20l,nyunyiza hizi kwa mpishano Rudia tena kila siku kumi hadi 14.zingatia inzi wa matunda huwa tunatumia mitengo kwani kuwaua kwa siku ni changamoto sana kwaiyo tunatumia mitego kama ukihitaji tunayo ekari moja utahitaji mitego 4.

 

NO4: KUDHIBITI MAGONJWA

 Kipindi cha kutoka majani, maua na matunda tumia dawa yenye kiambata cha thiophanate na methyl  ya unga.matumizi changanya 50gram/20l sawa na vijiko vitano vya chakula pulizia kila siku 14 . iwapo kutakuwa na tishio la mabaka meusi  katika majani  dawa yenye kiambata cha propineb na metalaxyl 50g/20l itatumika kila siku 14 piga kwa mpisha wiki hii ukipiga hii wiki ijayo unapiga hii

KWA MAITAJI YA MITEGO YA NZI WA MATUNDA WASILIANA NASI 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.