kilimo cha papai

kilimo cha papai

papai ni zao la kitropiko ambalo huhitaji joto la wastani kati ya nyuzi 25 na 30 za Sentigredi na mvua kiasi cha milimeta 1,000 na 1,800 kwa mwaka.Zao hili linastawi vizuri kwenye udongo usiotuamisha maji

aina za mbegu za papai

SINTA F1

  • Hukomaa kwa muda wa miezi 7-9
  • Huweza kuvumilia magonjwa ya virusi
  • Rangi yake ya ndani ni njano
  • Mmea wake ni mfupi
  • Uzito wa tunda ni kilo 2 mpaka2.5

RED ROYALE F1

  • Hukomaa kwa miezi 7-9
  • Inavumilia magonjwa ya virusi
  • Mmea wake ni mfupi
  • Rangi ya ndani ni nyekundu
  • Uzito wa tunda ni 1.5 mpaka 2.

 

CARINA F1

  •  Hii ni mbegu ya hybrid yenye rangi ya nyekundu
  •  Mmea wake ni mfupi tunda lina rangi nyekundu
  •  Tunda linauzito wa kilo 1.5-2kg
  •  Linakiwango cha sukari kiasi cha 14%
  • Inavumilia magonjwa ya virusi kama papaya ring spot virus

 

MALKIA F1 HYBRID

  • Uzalishaji wake ni wa hali ya juu. Unaweza kuvuna matunda 30 hadi 40 kwa msimu
  • Mti wake ni mfupi wa wastani na huanza kutoa matunda unapofikia urefu kuanzia sentimeta 50 hadi 80
  • Matunda yake ni manene,magumu na yenye uzito wa kuanzia kilogram 1.5 hadi kilogramu 2, pia yana uwezo wa kukaa muda mrefu bila kuharibika na yanafaa kwa usafirishaji wa umbali mrefu
  • Tunda lake lina ubora mzuri, Na nyama yake ni nyekundu lina ladha zuri na tamu pia ina kiasi kingi cha sukari kuanzia 13-14% asilimia (sugar content)
  • Mapapai jike tunda lake ni fupi na pana wakati mwingine matunda yake ni marefu
  • Maua huanza kutoka baada ya miezi mitano tangu kupandwa, matunda yanaweza kuvunwa baada ya mienzi 10 hadi 11 tangu kupandwa au kutegemea hali ya hewa
  • Pakiti ya gramu moja ina jumla ya mbegu 50 hadi 60 (kutegemea na ukubwa na uzito wa mbegu ),Heka moja inahitaji gramu 50 hadi 80 za mbegu
  • Papaya Malkia inastahimili magonjwa ya virusi (papaya Ringspot Virus )

 

jinsi ya kuotesha mbegu za papai.Ili mbegu zilizo kavu za papai zipasuke na kuota zinahitaji vitu zifuatavyo.Mwanga wa jua wa kutosha hali joto,unyevunyevu.hatua za kuotesha.

1. Fungua pakti yako ya mbegu.

2. Weka maji kwenye chombo  chochote na uloweke mbegu kwa muda wa siku 3 (saa 72). hakikisha unamwaga maji na kuweka mengine kila baada ya saa 24.

3. Baada ya saa 72 kupita, chukua kitamba na weka mbegu zako zote kwenye kitamba na kuzifunika vizuri.

4. Chimba shimo dogo kwenye sehemu ya mwanga wa jua wa kutosha, kisha weka mbegu ulizofunika kwenye kitamba na kuzifukia.

5. Mwagilia maji kila siku sehemu ya juu uliyofukia mbegu. itachukua siku 8 mpaka 12 mbegu kupasuka kutegemea na halijoto.

6. Mbegu zikipasuka unazihamishia kwenye kitalu au tray ya kupandia mbegu au kwenye viriba (polythene tube). katika hatua hii tumia kijiti au kitu chenye ncha kali katika kupanda mbegu. Hii inasaidia kuepuka kuvunja maotea ya mbegu.

7. Hakikisha unaweka mbegu si kwa kufukia sana. weka mbegu juu juu na fukia kwa kiasi kidogo sana udongo. Mara nyingi mbegu za papai hazina nguvu sana za kusukuma udongo kama utazifukia sana.

8. Baada ya kuweka mbegu, chukua mfuko wa sandarusi (jute bags) na  funika juu ya kitalu tafadhari usitumie majani makavu katika hatua hii.

9. Mwagilia maji kwa siku mara moja juu ya mifuko ya sandarusi kwa muda wa siku 3-5 mbegu zitaanza kutoa majani ya awali.

10. Baada ya siku 6-7 ondoa mifuko ya sandarusi.

11. Mbegu zikifikia sm 8-10 unaweza kuhamishia kwenye mashimo shambani

UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA PAPAI
Hustawi vizuri katika udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH ya 6 hadi 7.hukubali katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.unaweza kulima katika udongo wa kichanga au Tifutifu japokuwa katika udongo wa mfinyazi kama mvua itakuwa kubwa na maji yakatuama kwa muda mrefu huzuia ukuaji mzuri wa papai

SOIL PH

pH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7. Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).papai hustawi kwenye udongo wa tifutifu wenye tindikali ya wastani na virutubisho vya kutosha.

Maandalizi ya  shamba:

Shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupanda. Wakati wa kutayarisha shamba punguza miti, ng’oa visiki na fyeka majani, halafu yakusanye pamoja na yachome.Chimba mashimo yenye ukubwa wa sentimeta 40 upana, urefu na kina. Nafasi kati ya shimo na shimo iwe meta mbili au tatu na mstari na mstari iwe meta mbili na nusu hadi tatu. Baada ya kuchimba mashimo jaza mbolea ya samadi au takataka zilizooza vizuri kiasi cha debe mbili kwa kila shimo.

JINSI YA KUANDAA MASHIMO YA KUPANDIA PAPAI

1. chimba shimo kwa ajili kupanda mpapai, liwe na kina cha sm.60 na upana sm 40-60.

 2. udongo unatakiwa utenge katika makundi mawili ule wa kwanza kutoa weka upande wake na ule wa mwisho weka upande wake hii itakusaidia wakati wa kuweka mbolea na mboji.

 3. chini kabisa ya shimo unaweza kuanza majivu then unaweka ule udongo wa kwanza kabisa kutoa kidogo tu baada ya hapo

4. unaweka nyasi kavi zilizokauka vizuri hii itakusaidia kuwa na utajiri wa viritubisho kwenye shimo lako la papai kwani nyasi kavi ukifukia na udongo unatengeneza mboji. ukishaweka nyasi kiasi fukia na udongo ule ule wa mwanzo kuhutoa kwenye shimo. weka kiasi

 5.malizia kwa kuweka mbolea ya samadi debe moja iliyokauka vizuri yaani mbolea ambao iko tayari kutumiwa kwa ajili ya matumizi ya mashambani baada ya kuweka mbolea weka ule udongo wa mwisho kuhutoa kwenye shimo weka kiasi tu baada ya hapo mwagia maji kwa kipindi chote mpaka pale utakapopanda  miche yako  kwani kuanda shamba mapema kuna faida kubwa sana

 6.baada ya kuweka  mbolea ya samadi hatua inayofuata ni kupanda miche yako kutoka kwenye viriba ni vyema kuhamisha miche kipindi cha jioni hatua za ukuaji wa mpapai Kitalu – Wiki 1 – 6 Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa shambani – wiki 7 -16 Maua na kuweka matunda – wiki 17 – 21Kukua kwa matunda – 22 – 26Mavuno ya kwanza – Wiki 37 nakuendelea

 SABABU YA MMEA WA PAPAI KUWA DHAIFU NA KUANGUSHA MAUA.

  • hali ya hewa Joto likiwa juu sana hupelekea sana maua kuanguka na pale ambapo joto hushuka chini sana pia hupelekea kuanguka.

  • wadudu na magonjwa Maua huanguka kwa kupata usumbufu wa wadudu na magonjwa

  • kutomwagilia maji ya kutosha

  • ukosefu wa nitrogeniMmea hutaji nitrogen kwa ajili ya kutengeneza maua na majani kuwa yenye afya kwa ajili ya kuimarisha mmea kwa mmea kukosa kiasi cha kutosha cha naitrojen pale ambapo maua yatajitegeneza yataishia kuanguka kwani yatakuwa dhaifu.

  • mche kutoa maua mengi.Hutokea Mara kwa Mara mche kutoa maua mengi sana kwa wakati wa kutengeneza maua na pia hutokea pale uwekaji wa mbolea za naitrojeni unapokuwa mkubwa.

  •  Mmea kukosa mwanga wa kutosha Vitu ambavyo huchangia sana ukuaji mzuri na hatimaye mmea kuweka maua katika mche ni pamoja na mwanga wa kutosha ambao husaidia sana kwa maua kutoa mbali na hapo mkulima hataendelea kuona tatizo /changamoto hii katika kilimo Papai 

 

SABABU YA MATUNDA YA PAPAI KUDONDOKA MACHANGA?

Ardhi ikiwa na kiwango kidogo cha magneziamu (Mg) pia ikiwa na kiwango cha juu cha Potasiam (P) na Boron (B). Hivyo kabla hujaandaa shamba kwa ajili ya kilimo cha papai ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu wa aina ya udongo ili upate uhakika wa kujua unachotaka kukipanda.Kuna wakati miti ya mipapai, hudondosha matunda wakati yakiwa bado machanga, kitendo ambacho ni hasara kwa wakulima.kudondosha matunda muda mfupi baada ya kuanza kuzaa na hii hutokea baada ya maua kujitenga na tunda.Hii imekuwa changamoto kubwa kwa wakulima na wengi wamekuwa wakiulizia kuhusu kadhia hii.Ili kuliweka sawa jambo hili, tutaongelea miti ya mipapai kupukutisha matunda ambayo hayajakomaa.

Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na hali ya hewa au mvua kuzidi, magonjwa ya mmea, wadudu au uhaba wa rutuba na mbolea. Pia uwekaji mbolea ya kukuzia katika kipindi kisichotakiwa.Miti ya matunda inapaswa kupata kiwango stahiki cha maji katika ukuzaji. Epuka kumwagilia kiasi kikubwa cha maji kwa kufikiri unafanya vizuri kwani hiyo inaweza kusababisha miti kudondosha matunda yakiwa machanga. Kumbuka kuwa miti ya mipapaia iliyokomaa haihitaji maji wakati wote.Kwa kawaida miti ya matunda hukua na kuzaa vizuri katika mazingira ya uoto wa kitropiki, mazingira ambayo kwa kawaida licha ya kupata mvua hayana baridi sana. Hata hivyo, mti uliokomaa unaweza kustahimili mazingira yalio na joto kidogo.Usiondoe majani wala matawi yaliyoanza kunyauka acha yadondoke yenyewe

 Matunda yakiwa madogo yanaweza kushindwa kustahimili kukua endapo hali ya hewa itabadilika kutoka joto kuwa baridi. Baridi huathiri kiini cha matunda katika mbegu hali ambayo husababisha tunda kuzalisha aina fulani ya gesi (ethylene) ambayo husababisha tunda kudondoka kabla ya wakati wake.Kumbuka mbolea ikizidi au kupungua inaweza kusababisha mti kudondosha matunda yake, hivyo ni vyema kuhakikisha unafuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuweka mbolea.

 Unashauriwa kutumia mbolea iliyo na virutubisho na kuthibitishwa kitaalamu kwa ajili ya miti ya matunda na iliyo na kiwango sahihi cha naitrojeni (N), Fosiforas (phosphorous.P) na Potasiam (K). Kwa pamoja madini haya huufanya mmea kupata virutubisho muhimu.

MUHIMU   

Zingatia sana katika uchaguzi wa aina ya mbolea; chagua mbolea ambayo ina kiwango kikubwa cha P na K ukichagua mbolea ilio na kiwango kikubwa cha Nitrojeni (N) hii inaweza kuharibu maua.Unaweza pia kutumia mbolea ya mabaki ya mimea na wanyama katika kukuza mipapai yako.Aidha, uongezaji mbolea kiholela pia unaweza kuathiri mmea.Ni muhimu kuzingatia sababu zinazosababisha mipapaikudondosha matunda kabla hayajakomaa, kwani matunda yanapondoka huchochea mti kuzalisha kemikali ya ethylene ambayo husababisha matunda mengine kuendelea kudondoka.

UWEKAJI WA MBOLEA   

Ili mimea iweze kukua haraka, inashauriwa kuweka mbolea za kukuzia kama vile CAN au Urea. Kiasi kinachotakiwa ni kilo kilo100 za kwa hekta moja. Mbolea za asili kama vile samadi na mbolea vunde ziwekwe kila mwaka kiasi cha kilo debe moja hadi mbili kwenye kila mpapai ili kuongeza ukuaji na uzazi. Mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na hii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

kwa maitaji ya Muongozo wa uwekaji mbolea katika mipapai wasiliana nasi 0717274387

 
 JINSI YA KUFANYA PALIZI

shamba la mipapai ni muhimu hasa wakati wa mwanzo. Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu. Magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu. Njia nzuri ni Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa. ondoa mipapai na upande mwingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe 

MAGONJWA YA PAPAI

Ubwiri unga 

ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu)hasa kwenye unyevunyevu wa (80-85%)na hali ya nyuzi joto kuanzia24-26°C..ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na  madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivukatika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani. 

TIBA NA KINGA
Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza sumu za ukungu zenye Hexaconazole kama vile MOVIL, na siku za upuliziaji itategemea muda  masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.

 2.Ugonjwa wa kujikunja na kudumaa majani

ni ugonjwa unaosababishwa na wadudu amabo wanaofyonza kama wadudu mafuta hueneza virusi ni ugonjwa  ambao huambatana na kujikunja kwa majani machanga na kuwa magumu  na mmea kudumaa kukua.

KUZUIA NA KINGA

Zibiti wadudu wanao eneza ugonjwa huu kwa kutumia madawa ya kuuwa wadudu kama vile   yenye kiambata cha cypermenthin144g/l+imidacloprid Pia tumia sumu za wadudu kuua wadudu kama wadudu mafuta  ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu kama RAPID ATTACK.

3.Ugonjwa wa manjano

Ni ugonjwa unasababishwa na virusi amabao mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.

KUZUIA NA KINGA

Zibiti wadudu wanao eneza ugonjwa huu kwa kutumia madawa ya kuuwa wadudu kama vile RAPID ATTACK au cypermenthin144g/l+imidacloprid Pia tumia dawa za wadudu kuua wadudu kama wadudu mafuta  ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu. 

Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa  sigara/tumbaku katika shamba la papai wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la papai.Ng'oa mimea iliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya papai.

4.Kuoza Shina 

Husababishwa na ukungu (fangasi) hasa kumwangilia maji kupita kiasi na hushambulia miche michanga. Miche iliyoshambuliwa huonyesha dalili za kunyauka, baadae huanguka na kukauka. Miche mikubwa huonyesha dalili za kudumaa. Sehemu ya shina iliyokaribu na ardhi hulainika na kuwa na rangi ya kikahawia. 

KUZUIA NA KINGA

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa Kwa kutumia njia zifuatazo Punguza miche Kama imesongamana Nyunyizia dawa za ukungu Kama vile Dithane M - 45, Ridomil, Thiophanate (Topsin - M)

5.Bakajani

Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda inayoshikana na kikonyo

KUZUIA NA KINGA

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa Kwa kutumia njia zifuatazo kupanda mbegu bora zinazokizana na ugonjwa au Nyunyizia dawa za ukungu Kama vile supergrino,movil

6. Chule

Huu ni ugonjwa wa ukungu unaoanzia kwenye mbegu husababishwao na fangasi (Colletotrichum spp). Ugonjwa huu huweza kushambulia zao ya papai katika hatua zote za ukuaji hata baada ya kuvuna na mara nyingi hutokea wakati shamba linapokua katika hali ya unyevu mwingi.Ugonjwa huu husababisha madoa yaliyo bonyea yenye maji ambayo baadae hutanuka na kuwa meusi yenye viduara vya kahawia.

KUZUIA NA KINGA

Hakikisha unatumia mbegu safi zisizo na maambukizi ya ugonjwa na kufanya mzunguko wa mazao. Pandikiza miche isiyo na ugonjwa shambani kwa nafasi inayopendekezwa, kuepuka msongamano na pia usimwagie maji majani ya mimea kuepuka kuongeza hali ya unyevu . a dawa za ukungu zenye viambato vya Chlorothalonil, Mancozeb na Carbendazim. Mfano wa dawa za ukungu Dithane – M45(Mancozeb), Agrothalonil 720SC (Chlorothalonil) na Elcazim 50SC (Carbendazim).

7.Kuoza kwa china

Husababishwa na kuzidi kiwango cha maji hasa kwenye shina na mizizi hasa kumwangilia maji kupita kiasi na hushambulia miche michanga. Miche iliyoshambuliwa huonyesha dalili za kunyauka, baadae huanguka na kukauka. Miche mikubwa huonyesha dalili za kudumaa. Sehemu ya shina iliyokaribu na ardhi hulainika na kuwa na rangi ya njano. 

KUZUIA NA KINGA

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa Kwa kutumia njia zifuatazo Punguza miche Kama imesongamana Nyunyizia dawa za ukungu Kama vile Dithane M - 45, Ridomil, Thiophanate (Topsin - M)

 

 ujuzi kilimo 

 HATUA YA TATU MPAPAI UMEFIKISHA MWEZI MMOJA

NPK 15-9-20 +1.8 MgO, +9.5 SO3, +0.015 B, +0.02 Mn, +0.02 Zn.

Weka mbolea ya kukuzia ya NPK baada ya mwezi mmoja weka gram 10 sawa kijiko kimoja cha chakula au

Weka mbolea ya ujazo wa kifuniko cha maji ya uhai viwlili /kijiko kimoja kidogo cha chai viwili sawa na gramu kumi katika kila shina la mche mmoja

Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia zingatia kuweka mbolea hii mapema

 

HATUA YA NNE MIPAPAI IMEFIKISHA MIEZI 2

NPK 15-9-20 +1.8 MgO, +9.5 SO3, +0.015 B, +0.02 Mn, +0.02 Zn.

Weka mbolea ya kukuzia ya NPK baada ya miezi miwili weka gram 20 sawa na vijiko 2 vya chakula au

Weka mbolea ya ujazo wa vifuniko vya maji ya uhai vinne/kijiko kidogo cha chai vinne sawa na gramu ishirinii katika kila shina la mche mmoja

Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia zingatia kuweka mbolea hii mapema kabla ya kutoa maua

HATUA YA TANO MIPAPAI IMEFIKISHA MIEZI 3

NPK 15-9-20 +1.8 MgO, +9.5 SO3, +0.015 B, +0.02 Mn, +0.02 Zn.

Weka mbolea ya kukuzia ya NPK baada ya miezi mitatu weka gram 30 sawa na vijiko 3 vya chakula au

Weka mbolea ya ujazo wa vifuniko vya maji ya uhai sita/kijiko kidogo cha chai sita sawa na gramu 30 katika kila shina la mche mmoja

 

kwa maitaji ya muongozo wa uwekaji mbolea na uzibiti wa visumbufu vya mimea ya papai wasiliana nasi tukutumie kitabu cha muongozo kulingana na kanda husika 

 

  • +255717274387/+255759417639

  • Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

 

Habari? kangeta kilimo APP humsadia mkulima na mfugaji kutatua tatizo la magonjwa, Wadudu, magugu, masoko kwa urahisi kupitia simu yake ya mkononi download ???????? now

 

 

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.