kilimo cha nyanya

viwavi jeshi vamizi(fallarmyworm)

Viwavi jeshi vamizi ni wadudu waharibifu ambao walianza kuonekana Afrika Mashariki kuanzia mwaka 2016.Wanaweza kuwa na rangi nyeusi, kahawia au kijani

Wanakula mimea zaidi ya aina 80.Wanaharibu zaidi mimea jamii ya nafaka ingawa mazao hayo yakiwa hayapo wanaharibu sana pamba.

Asili na Usambaaji wa Kiwavi jeshi vamizi (Fall Armyworm)

  • Asili yake ni Amerika ya kati na kusini a -Machi, 2017
  • Mwaka 2016 alionekana nchini NIGERIA
  • Zaidi ya nchi 20 za Afrika zimevamiwa na mdudu huyu
  • Tanzania alionekana katika mikoa ya Ruvuma,Rukwa na mbeya mwaka 2017
  • Zaidi ya mikoa 20 TZ imeshavamiwa na FAW-Machi, 2018

 MZUNGUKO WA MAISHA  YA KIWAVI JESHI VAMIZI  (FALLARMYWORM

 

 TABIA ZA NONDO WA KIWAVI JESHI VAMIZI

  • Huonekana kwa urahisi nyakati za usiku
  • Ana uwezo wa kuruka umbali kilometa 100 kwa usiku mmoja
  • Anataga mayai 50-200 kwa mafungu
  •  Mayai hufunikwa na utando mweupe
  •  Mayai huanguliwa kati ya siku 2 hadi 5 kuwa funza
  •  Funza  hutapakaa kwenye majani na huanza kula majani upande wa chini ya mmea
  •  Funza ni waharibifu  zaidi  muda wa asubuhi sana na jioni
  •  Funza hutoa kinyesi kinachomkinga asiliwe na wadudu wengine au sumu isiweze kumfikia

 NJIA ZA KUDHIBITI  NONDO NA FUNZA WA KIWAVI JESHI VAMIZI

Kagua shamba lako mara kwa mara ili uweze kutambua kama nondo, mayai, funza au viashiria au dalili za uharibifu katika zao la mahindi na mimea ya nafaka au mipamba na uchukue hatua zinazostahili  Kinga mazao kwa kutumia njia za kiutamaduni mfano, weka shamba katika hali ya usafi,tumia mbegu inayokinzana na nondo wa kama zipo, kilimo cha kubadili mazao au kupanda mimea inayozuia wadudu wasiingie shambani Ondoa masalia ya mimea ya mimea baada ya kuvuna na choma moto   Tumia mitego yenye mtego wa maji yenye harufu ya kipepeo jike, hivyo kuwa na uwezo wa kuvutia madume na mara yanapoingia yanakufa.

 

 

 VIUADUDU VINAVYOWEZA KUDHIBITI KIWAVIJESHI VAMIZI

  • Alpha-cypermethrin 10EC (systemic)
  • lambda-cyhalothrin 5 SC au 100CS (Contact)
  • Indoxacarb 14.5 EC au 150 EC/SL    (Contact)
  • Lufenuron 500 EC (Contact)
  • Deltamethrin 2.5 EC (Contact)
  • Profenofos 500 EC au 720 EC (Contact)
  • Acetamiprid 200 SC (Systemic)
  • Acetamiprid + Lambda-cyhalothrin 60EC (Syatemic + contact)
  • Imidacloprid + Emamectin benzoate 175SC/WDG (Systemic + contact)
  • Emamectin Benzoate + Alphacypermethrin 150 EC (Contact + systemic)
  • Profenofos+ Lambdacyhalothrin 315 EC/ULV (Contact)
  • Flubendiamide  480 SC  (Systemic)
  • Malathion 50 EC (Contact)
  • Emamectin Benzoate 10 EC au 16EC (Contact)
  • Cypermethrin+chlorpyrifos 450 EC (Contact)
  • Cypermethrin+Imidacloprid 344 SE (Contact + systemic)

UTARATIBU WA KUNYUNYUZIA VIUADUDU VINAVYODHIBITI NONDO WA KIWAVI JESHI VAMIZI

  • Pima kiwango sahihi cha kiuadudu kama ilivyoelekezwa kwenye kibandiko na kuchanganya kwenye ujazo wa maji uliopendekezwa
  • Nyunyizia viuadudu mara tu unapoona dalili na viashiria vya kuwepo kwa nondo, mayai na viwavi katika shamba . Rudia unyunyizaji wa viuadudu mara unapoona viashiria na dalili za kuwepo kwa kisumbufu katika shamba .
  • Nyunyiza asubuhi sana au muda wa jioni ambapo nondo wa kiwavi jeshi huonekana kwa urahisi au funza wanaweza onekana kwa urahisi kwenye majani na mashina
  • Epuka kunyunyiza kiuadudu kukiwa na upepo mkali au  mvua kwani huwa vinapunguza uwezo wa sumu kufanya kazi iliyokusudiwa
  • Ni vyema kuwa na utaratibu wa kunyunyizia mashamba yaliyo karibu na shamba lako ili kuepuka mashamba yasiyonyunyiziwa viuadudu kuwa mazalia ya nondo wa kiwavi jeshi vamizi

Angalizo: Viuatilifu ni sumu, unapovitumia ni vyema ukavaa vifaa kinga, kusoma kibandiko, kupima kiwango sahihi, muda wa kunyunyiza na muda wa kusubiri tangu uliponyunyiza kiuatilifu hadi kipindi cha kuvuna mazao. Pia usinyunyize kiuatilifu karibu na vynzo vya maji au sehemu ambazo kuna makazi ya  nyuki

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.