KULEA VIFARANGA ULISHAJI VIFARANGA/CHANJO/DAWA.

KULEA VIFARANGA ULISHAJI VIFARANGA/CHANJO/DAWA.

ULISHAJI VIFARANGA   Ili vifaranga wawe na maendeleo mazuri ya ukuaji, wanatakiwa wapewe chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ambavyo ni Protini, Madini,

Wanga na Vitamin pamoja na maji safi wakati wote.Hapa ndipo wafugaji wengi hukosea wanapo wapa vifaranga lishe duni na mwisho wa siku hudumaa na kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa.

  • Chakula cha kuku huendana na umri wa kuku kwa Vifaranga unaweza ukachanganya mwenyewe au ukanunua dukani
  • Ukichanganya mwenyewe hakikisha unatumia formula yenye uhakika itakayo kuwa na matokeo mazuri
  •  Hakikisha vyombo vya maji vinakuwa safi wakati wote.
  •  Chakula na maji yabadilishwe kila baada ya masaa 24.
  •  Hakikisha vifaranga wanapewa chakula wanachoweza kumaliza katika masaa 24 ili kuzuia uharibifu na mMang'alilachafua na kula tena uchafu na hatimae magonjwa.Hii ni mfano wa formula unayo wenza kuitumia kwa Vifaranga wa kienyeji katika miezi 2 ya mwanzo.

MIEZI MIWILI YA MWANZO.

  1. Unga wa dona wa nafaka kama mahindi  au mtama 40kg
  2.  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27kg Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20kg
  3.  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25kg
  4. Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10kg
  5.  Chumvi ya jikoni 0.5
  6.  Virutubisho (Broiler premix) 0.25

  JUMLA = 100kgs.

Vifaranga wapewe maji safi , vyombo vya maji visafishwe mara tu maji yatakapo chafuka Kila asubuhi sehemu zilizo na vyombo vya maji zikaguliwe na takataka zenye unyevu nyevu ziondolewe ili kudhibiti bacteria kuzaliana na Wageni wasiingie ovyo kwenye banda la Vifaranga

Kama una kuku wa kubwa anza kwanza kusafisha banda la Vifaranga ndio lifuate la kuku wakubwa

Kwa Vifaranga wa broiler wiki mbili za mwanzo utawapa chakula aina ya broiler starter

Kwa Vifaranga wa kienyeji, kisasa wa mayai (layers) au chotara (hybrid);utawapa Chick starter. Wiki ya  1 hadi 8

Vyombo vya chakula na maji unaweza ukatengeneza mwenyewe au ukanunua kitu cha muhimu ni kuhakikisha vinakuwa safi/ maji hayavuji/ vina kiwango cha kusaidia ulishaji vzur

CHANJO NA DAWA

Ni wazi kuwa hatari kubwa inayowakabili wafugaji wengi na hasa pindi wanapolea  vifaranga ni magonjwa.Yapo maradhi mengi ya vifaranga ambayo ndio changamoto kuu kwa kulea Vifaranga na kuku kwa ujumla na ndio chanzo cha miradi kufa na wafugaji kukata tamaa. Na ukikataa tamaa katka ufugaji huwez kufanya chochote kile maana utahisi kila mara unaingiza hasara kumbe ni wewe kukosa kuwa na lengo thabiti la ufugaji.

CHANJO NA KINGA ZA MUHIMU KWA KUKU WA MAYAI(LAYERS), CHOTARA, KIENYEJI.

1. Baada ya kuanguliwa

Chanjo ya Marek's

Dawa HVT

Namna: sindano

 2. Siku ya 2 hadi 6

KINGA ya Pullorum

Dawa: Trimazine 30%  plus Vitamin

Namna: Maji

 3. Siku ya 7

Chanjo ya Mdondo/Kideri (Newcastle)

Dawa: Newcastle vaccine [LASOTA]

Namna: Maji

 4. Siku ya 14

Chanjo ya Gumboro

Dawa: chanjo ya Gumboro

Namna: Maji

 5. Siku ya 16 - 20

KINGA ya Koksidiosis (coccidiosis)

Dawa: Trimazine 30% plus vitamin (Vitalyte itafaa)

Namna: Maji

 6. Siku ya 21

Chanjo ya Mdondo tena.. [Maelezo yapo kwa juu]

7. Siku ya 28 rudia chanjo ya gumboro

&Siku ya 30hadi 32

KINGA: kuimarisha kinga ya mwili

OTC 20% changanga na Amin'Total vitamin

8. Siku ya 35 hadi 39

KINGA: Mafua

OTC 50% au CORDIX (ukiona kinyesi kina muharo kiasi) au Tylosine 75% changanya na Amin'Total.

9. Siku ya 56

Chanjo: Ndui. Hapa inabidi uangalie sasa kutokana na changamoto za magonjwa wape kati ya wiki ya 7 na kuendelea kutokana na kwamba ktk majumba yetu tuna kuku wakubwa na wadogo hivyo tafiti zinasema hivyo kwa sasa.

10. Siku ya 60 hadi 64 (Rudia namba 7 hapo juu)

11. Wiki ya 12 ( kati ya siku ya 64 hadi 70)

Chanjo: Typhoid

12. Wiki ya 13 (kati ya siku 85 hadi 91)

KINGA: minyoo

13. Wiki ya 15

Ukataji wa midomo

14. Wiki ya 16

KINGA ya kipindupindu

OTC 20 YA SINDANO

Sindano kwenye nyama ya kifua.

15. Wiki ya 17

KINGA ya mafua

Tylosine ya sindano

Sindano kwenye nyama ya kifua

16. Wiki ya 18

chajo ya Typhoid

Baada ya hapo, waache kuku.. Hakuna sindano tena...

&Chanjo zinazobaki ni...

(A) Mdondo/Kideri(Newcastle Vaccine) aina ya LASOTA

(B) Minyoo

&Hizi zote ni kila baada ya miezi mitatu mitatu........

KULEA VIFARANGA NA SABABU ZA VIFO KWA VIFARANGA.

Hii ni sehemu  katika somo la kulea Vifaranga, naamin kila mtu anafahamu nini maana ya banda la Vifaranga, vitu vya muhimu katika mabanda ya vifaranga, maandalinzi ya kupokea Vifaranga, kulisha Vifaranga/ chanjo sasa tuendee na hii sehemu ya sababu ya vifo kwa Vifaranga"Kulea Vifaranga ni moja ya kitendo ambacho wengi hukiogopa kwasababu ya vifo vingi kutokea!Katika kulea Vifaranga kuna hatua kama mbili ambazo vifo vinaweza kutokea

WAKATI WA KUSAFIRISHA VIFARANGA.

Hatua hii kuna vifo vinaweza kutokea ila sio kwa uhakika ni Mara chache sana, na hii husababishwa na kuweka vifaranga wengi kwenye box dogo, kubanana, kukosa hewa. Hata hivyo katika Hatua hii Vifo vya Vifaranga ni vichache mno na Mara nyingi Vifaranga hufika salama.

WAKATI WA KUVILEA VIFARANGA.

Hapa ndio kwenye changamoto na sababu za Vifaranga kufa, wakati wa kulea Vifaranga ndio vifo vingi hutokea.

Na kutokea kwa vifo hivyo tambua kuna sababu zinazo sababisha Vifo kwa vifaranga kutokea.

Baadhi ya sababu za Vifaranga kufa ni hizi

a• Vyanzo vya Vifaranga

b • Usimamizi mbovu

c• Lishe duni

d• Magonjwa

(A) VYANZO VYA VIFARANGA.

Wakati  wa kununua  vifaranga unatakiwa ununue kwenye vyanzo salama vinavyotoa Vifaranga bora, waliochangamka, wasio na magonjwa, ulemavu mwenye maji ya kutosha mwilini.Tambua sehemu za kutotoleshea vifaranga zinaweza kuwa chanzo cha vifo kwa Vifaranga kama watakuuzia Vifaranga wasio na ubora, mwenye ugonjwa kwa mfano  ugonjwa wa Kuharisha Kinyesi Cheupe (Bacillary White Diarrhea)Ni ugonjwa wa kuku unaosababishwa na bakteria na hushambulia zaidi kuku wadogo wenye umri hadi wiki tatu.

Ni moja ya magonjwa yanayo shambulia sana Vifaranga, na kuna uwezekano mkubwa kununua Vifaranga wakiwa na ugonjwa huu, kama sehemu ulipo nunua Vifaranga si salama ,kwani  Maambukizi ya ugonjwa huu yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na vifaranga kuathirika.

(B) USIMAMIZI MBOVU

Hapa sasa ndio kwenye kiini cha sababu za vifo kwa Vifaranga, usimamizi mbovu unaweza changia kiasi kikubwa Vifaranga kufa

 ( 1) Vyombo vya maji

Hapa Vifaranga hufa hasa siku za mwanzo kama huto weka kokoto ndogo ndogo kwenye chombo cha maji ili watakapo kuwa wanakunywa wasilowe au kuzama kabisa kwenye maji kuna weza pelekea Vifaranga kufa.Na kwawale ambao hutengeneza vyombo vya maji wenyewe vinakuwa na kina kirefu hivyo hupelekea Vifaranga wakati wanataka  kunywa  maji huzama na hatimaye kufa.

  • Vyombo ya maji vinatakiwa viwe safi muda wote hakikisha una badilisha maji kwa siku mara moja au mbili pale tu utakapo ona yamechafuka
  • Hakikisha maji hayavuji na utakapo ona yamevuja safisha haraka kwani unyevu nyevu ni hatari kwa Vifaranga na kuna uwenzakano mkubwa kusababisha  Bacteria kuzaliana.

(2) VYOMBO VYA CHAKULA

  1. Vyombo vya chakula vinahitajika viwe vingi kutegemea uwingi wa Vifaranga, pia kuna wengine hutumia sahani au magazeti kuwekea chakula njia hiyo inaweza rahisisha sana Vifaranga kuambukizwa magonjwa kupitia kinyesi.
  2. Kwasababu  wakati vinakula huingia ndani ya chakula na kama kuna kifaranga mgonjwa kinyesi chake kikichanganyika na chakula , ikatokea kifaranga mwingine akala chakula hiko kilicho changanyika na kinyesi cha kifaranga mgonjwa itakuwa ni rahisi sana ugonjwa kuenea bandani kwa muda mfupi.
  3. Pia hakikisha vyombo vya chakula vinakuwa safi, chakula kibadilishwe wakati wa kueka chakula kingine, una shauriwa kuweka chakula kidogo kulingana na uwingi wa Vifaranga ili kupunguza utupaji wa chakula kitakacho baki &Kwasababu haitakiwi chakula kilicho baki cha leo kichanganywe na kingine kesho, ila chakula kitakacho baki unatoa una weka kingine.

(3) BARIDI NA JOTO WAKATI WA KULEA VIFARANGA

Hii ni moja ya sababu inayo weza kudumaza Vifaranga pale tu watakapo kosa joto la kutosha ,au inaweza kuuwa Vifaranga pale joto litakapo zidi na kusababisha Vifaranga kukosa maji na hatimaye kufa au  pia Vifaranga vinaweza kufa kwa kwasababu ya baridi Vifaranga kulaliana sehemu moja vya chini vitakosa hewa na hatimaye kufa.

  1. Hapo utakuwa umeshaelewa kuwa joto likizidi kuna madhara yake
  2.  Na baridi pia ina madhara yake kwa Vifaranga

Kitu cha muhimu ni kuchunguza mijongeo ya Vifaranga wako ndio itakayo kufahamisha kuwa joto limezidi au la!

 Ufuatiliaji wa karibu utamsaidia kuchukua hatua

mapema endapo marekebisho yatahitajika. Hii utafahamu kwa kuangalia tabia ya vifaranga wanapokuwa ndani ya bruda

Kama joto linatosheleza utaona yafuatayo

  1.  Vifaranga vitalia kwa furaha,
  2. Vitakimbia kimbia,
  3. Vitakunywa maji,
  4. Vitachaguachagua takataka na
  5. Kuonyesha shughuli nyingi, zote hizi ni dalili nzuri kuwa joto linatosha.

Kama joto halitoshi utaona yafuatayo.

  • Vifaranga wakiona baridi , hujikusanya karibu zaidi na chanzo cha joto.au wao wenyewe hujikusanya pamoja kwenye pembe ya bruda au nyumba na hulia kwa sauti. Ukiona hivi ongezakiwango cha joto adi waonekane kutawanyikakote kwenye bruda.Kama joto likizidi utaona yafuatayo
  •  Vifaranga wakikaa mbali na vifaa vya joto ni dalili kuwa joto limezidi.
  • Joto likiwa kali vifaranga hukimbia kutoka kwenye mwamvuli (kama umewekwa).
  •  Husinzia na huzubaa.Katika hali hii itabidi upunguze joto kwa kupandisha taa juu na kama bado joto ni kalipunguza vifaa vya joto na kuwapa vifaranga maji mengi ya kunywa.Kama kutakuwa na upepo unaopuliza kutoka upande mmoja utaona yafuatayo
  • Vifaranga watajikusanya upande mmoja wa kitalu/bruda mbali na upepo unakotokea.Kutegemeana na jinsi utakavyowaona vifaranga wanafanya, kama wataashiria tatizo, fanya marekebisho mapema kabla hayajatokea madhara kwa vifaranga.Ndimi Mtumishi Wenu,

   Dr. Amani Lugano Mang'alila

  •  +255717274387/+255759417639
  •  Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

     

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.