Kuna aina mbalimbali za inzi wa matunda wanaoshambuliwa mazao mbalimbali kama maembe,matikiti,ndizi,papai,machungwa,parachichi nk, kangeta kilimo kitengo cha tafiti za visumbufu vya mazao
https://kangetakilimo.co.tz/pembejeo-za-kilimo
tumefanya tafiti mbali mbali za kuwasaidia wakulima nchini Tanzania kukabiliana na nzi wa matunda kangeta kilimo tumefanya tafiti na kuona kuna aina 4 za Nzi wa matunda ambao husumbua mimea jamii ya matunda kwa kiwango kikuwa ambao ni
1) NZI WA MAEMBE (Ceratitis cosyra)
Nzi huyu hushambulia sana maembe na muenekano wake ana mwili Ana mabawa yenye rangi ya manjano na kwenye mzunguko wa kifuani mwake kuna madoa meusi:urefu wa mabawa yake ni milimita nne hadi sita.sema inzi huyu hufanana sana na nzi wa mediteranean(ceratitis capitata) rangi na maumbile ya mabawa .Nzi huyu ameenea maeneo mengi ya Tanzania nzima na hushambulia sana maembe ,mapera ,manula nk
2) NZI WA NATAL (Ceratitis rosa)
Nzi wa natal anasifa ya kuwa na mabawa yenye mabaka ya kahawia na mabawa matatu sehemu ya nyuma ya kifua chake pia dume anamanyoa sehemu ya kati ya miguu yake.
Mzunguko wa maisha yake huanzia kwa nzi jike kutaga mayai kumi hadi ishirini ndani ya maembe na matunda mengine kwa wakati mmoja hutanga mayai kwenye matunda yaliyokomaa na yaliyoiva mayai yake huanguliwa ndani ya siku nne baada ya kutagwa funza hupitia hatua tatu na kuwa nzi kamili kwa muda wa siku kumi na mbili buu huchukua siku kumi na mbili hadi ishirini ndani ya udogo kabla ya kuwa nzi kamili nzi wa natal hushambulia matunda mengi kama papai,maembe,parachichi,mapera,kahawa
NZI wa natal anawezo mkubwa sana wa kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa hasa sehemu za joto na baridi anauwezo wa kuhimili sana mabadiliko makubwa ya hali ya joto kutoka sehemu za tropiki hadi sehemu zenye nyuzi joto chini ya sita za sentigredi
NZI WA MEDITERRANEAN(CERATITIS CAPITATA)
Nzi wa Mediterranean ameenea sana dunia nzima inzi mpevu wa Mediterranean ana urefu wa milimita tatu hadi tano Nzi huyu ana anarangi ya manjano na kahawia kwenye sehemu za tumbo na miguuni mwao pia anamabaka kwenye mbawa zake na macho yake yana rangi nyekundu yaliyochanganyika na zambarau nzi dume anavinyoleo viwili vyenye virungu nchani mbele ya kingo za macho yake
Nzi wa Mediterranean hukamilisha mzunguko wa maisha yake ndani ya siku 30 na anauwezo wa kutaga mayai matatu hadi kumi ndani ya tunda anauwezo wa kutanga mayai 20 kwa siku na mayai 870 katika maisha yake anashamulia matunda mengi sana kama maembe ingawa athari yake kwenye maembe sio kubwa sana kama kwnye kahawa ,machungwa,na ndizi
Kuna aina mbalimbali za inzi wa matunda wanaoshambuliwa mazao mbalimbali kama maembe, kangeta kilimo kitengo cha tafiti za visumbufu vya mazao tumefanya tafiti mbali mbali za kuwasaidia wakulima nchini Tanzania kukabiliana na nzi wa matunda kangeta kilimo tumefanya tafiti na kuona kuna Nzi wa matunda ambao husumbua mimea jamii ya matunda kwa kiwango kikuwa
NZI MVAMIZI (BACTROCERA INVADENS)
Nzi mvamizi hufanana sana na nyingu rangi ya mwili wake ni kahawia hadi nyeusi pembezoni mwa mwili wake anarangi ya kahawia na nyeusi .pembezoni mwa kifua chake kuna mistari miwili ya rangi ya manjano mabawa yake yana mistari miwili yenye rangi nyeusi upande wa chini na juu tumbo lake lina rangi ya machungwa na kifuani mwake kuna alama ya
Nzi huyu mvamizi hukamisha mzuko wa maisha yake ndani ya siku 22 hadi 30 anauwezo wa kutanga mayai 1000 katika mzunguko wa maisha yake.Nzi mvamishi ameeneoa sehemu kubwa mwa Tanzania na bara ya Africa .huyu ndie nzi anayeshambulia kwa kiwango kikubwa matunda aina nyingi sana kama jamii ya matango,maembe,machungwa, ndizi ,nyanya,kahawa,matunda ya porini,mapapi,parachichi,mapera huyu ndio nzi muharibufu kuliko nzi yeyote yule na husababisha harasa kwa kwa kiwango cha asimia 80.tunashauri wakulima kutumia juhudi ili kumzibiti huyu mdudu kwa kiwango kikubwa
MZUNGUKO WA MAISHA YAKE NA UHARIBIFU WA MBOGA NA MATUNDA
Mzunguko wa maisha yake huanzia kwa jike kutanga mayai ndani matunda na mboga mboga kama maembe ,bamia,mapera nk kwa kutumia mwiba mkali mwishoni mwa tumbo lake uitwao msinzi akiwa na umri wa siku tano hadi wiki nane mayai huanguliwa ndani ya tunda na kuwa funza ambao hukua ndani ya tunda (Embe)huku wakila nyama ya tunda au mboga na kusababisha tunda kuoza na kudondoka chini kisha funza kutoka ndani ya tunda na kujichimbia ardhini kiasi cha sentimita mbili hadi tano na kuwa buu matunda yaliyoshambuliwa kwa kila tunda moja linaweza kuwa na wastani wa funza 60 hadi 100 kwa kila tunda.mzunguko kamila
1. Yai huchukua siku mbili hadi tatu kuanguliwa kuwa funza
2. Funza huchukua siku tatu hadi tano kuwa buu
3. Buu huchukua siku tisa hadi kumi na mbili kuwa funa kamili
4. Nzi mpevu huishi kwa wastani wa siku 40
NJIA TUNAZOPENDEKEZA KUZIBITI NZI AINA YA NZI WA
Njia tunapendeka kuzibiti Nzi wa maembe aina ya Ceratittis cosyra ni kutumia njia za IPM kama kutumia mitego aina ya kangeta fruitfly aina ya augmentorium,pia unaweza kutumia njia ya kuweka chombo chenye protini kuweza kukamata madume pia udhibiti kibailogia matumizi ya viumbe maalum Wadudu walangi(predators),vimelea(pathogens),manyingu(parasitoids) na maji moto