Kuhusu

Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia.

Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo wakulima wadogowadogo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.

Changamoto

Ulimwengu umefanya juhudi kubwa kupunguza umasikini. Mwaka 1990 asilimia 43% ya idadi ya watu katika nchi zinazo endelea  wanaishi chini ya dola 1 kwa siku. Mnamo mwaka 2010 idadi hiyo ilipungua  kwa nusu na kufikia asilimia 21.

Ingawa bado kuna idadi ya watu wafikao milioni 900 ulimwenguni ni wastani wa asilimia 70% ya idadi hiyo wanaishi vijijini, wengi wao bado wanafanya kilimo kwa ajili ya kula tu ili waweze kuishi.

Kangetakilimo imeona biashara ni njia nzuri ya kuondoa umasikini ambayo kila mtu anaweza kuishi na kuwa na hakiba. Kuinua kilimo ni njia muhimu katika kufikia malengo.

Fursa

Ingawa fursa ni nyingi ulimwenguni, asilimia 60% ya watu masikini ulimwenguni wanaishi Africa . Kiasi kikubwa cha ardhi ambayo haitumiki inapatikana Africa.

Wakati huo huo matazamio ni kwa idadi ya watu Africa ambayo inatalajiwa kuongezeka mara mbili ya billion mbili ifikapo mwaka 2050 . Ardhi na wafanyakazi vinapatikana . Changamoto moja itakuwa ni kutumia malighafi hii kufikia mahitaji yanayokua ya chakula .

Suluhisho linabaki katika kuongeza uwezo wa uzalishaji wa kilimo kulingana na  UNFAO. Africa inauwezo wa uzalishaji asilimia 24, America ya kati asilimia 35, na Asia ya kati asilimia 36. Ulimwengu umeoa kuna fulsa kubwa ya kilimo Africa.

Mapinduzi ya kilimo Africa yameendelea lakini mapinduzi haya ya kilimo yanajumuisha na kuwafaidisha masikini wanaoishi vijijini na mipakani mwa Africa.

Mnyororo wa thamani

Wakulima wa vijijini wa Africa  na nchi zinazoendelea wanapaswa kuwa ni moja ya sehemu ya suluhisho katika kuongeza uzalishaji na kuondoa umasikini vijijini. Kuna mitandao ya wakulima kulasa za facebook,twitter  na istagram, makundi ya watsapp kwa ajili ya wakulima kupata elimu na huduma kupitia kangetakilimo baada ya kuwa mwanachama na kuendelea kupata huduma bure.

Kutakuwa na mtandao wa kanda utakaoongozwa na wajasiliamali wadogowadogo na wazalisha ajira mbalimbali katika ngazi ya jamii.

Tunahamasisha  kubolesha maisha ya watu katika Nyanja zifuatazo;

 • Afya
 • Maji safi
 • Maswala ya fedha
 • Elimu
 • Msaada wa kitaalamu
 • Kujitambua/ kufahamu jambo
 • Kujua jinsi ya kuanzisha jambo
 • Kukuza uchumi.

Kangetakilimo hutoa msaada wa zaidi ya wadau 1000 wa Kangetakilimo Tanzania.Kangetakilimo imeanza kutoa huduma Tanzania mwaka 2018.

Dhumuni ilikuwa ni ;

 • Kusambaza mbolea za asili viwandani, viwatilifu,na mbegu kwa wakulima ,pasipo kutegemea mabenki au misaada mingine.
 • Kazi hufanywa na timu ya mameneja wanne wadogo wadogo
 • Na meneja mmoja mkubwa ikiwa imelenga hasa wakulima wadogo wadogo Tanzania.

 

Nini tunafanya

Kangetakilimo ni biashara yenye matawi mbalimbali ambayo inagusa mazingira na changamoto za kiuchumi katika Nyanja za chini. Kangetakilimo imeanzisha mpango endelevu na unaofata taratibu wa kuwafatilia wakulima kupitia, mitandao ya kijamii , youtube , mtandao wa simu.tofuti,nk

 

 Kangetakilimo inatoa huduma zifuatazo;

 1. Ushauli muhimu wa kilimo
 2. Semina za kilimo
 • Masoko ya kilimo ya Africa na nje ya Africa
 1. Tecknologia ya kilimo
 2. Kiwango cha ph ya udongo
 3. Mafunzo kupitia mashamba ya mifano.
 • Kangetakilimo inatengeneza nafasi mpya ya biashara.

 

Nini tunaamini

NDOTO ZA KINGETAKILIMO

Kangetakilimo imelenga kuanzisha kilimo bora cha uzalishaji wa mazao kwa kuhusisha matumizi ya tecknolojia ili kuongeza kipato, kuongeza virutubisho, upatikanaji wa chakula na masoko.

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.