UFUGAJI WA MBUZI NA KONDOO.

Kilimo cha Kabichi

Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya cauliflower kabichi  Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja,

lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka.

Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri. Kabichi ni zao linalopendelea hali ya ubaridi. Zao hili hustawi na kutoa mazao mengi na bora kwenye sehemu zenye miinuko ya kuanzia mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari.

Nchini Tanzania kabichi hustawishwa zaidi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Iringa na Mbeya. Kabichi ina madini aina ya chokaa, kambakamba, protini na maji kwa wingi. Mboga hii inaweza kuliwa bila kupikwa au kuchemshwa kwa kutengeneza kachumbari. Pia inaweza kupikwa pamoja na vyakula kama vile nyama na maharagwe

HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA KABECHI

Kwa kawaida kabichi huhitaji hali ya hewa iliyotulia na kavu ili kuweza kufanya vizuri. Lakini kabichi humudu mazingira mengi. Mazingira yenye baridi kali au joto kali huharibu ukuaji pamoja na uzaaji wa kabichi. Udongo wowote wenye virutubisho hai unafaa kupandia kabichi kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa udongo unaweza kuupa mmea chakula kiasi kinachohitajika kukua na kuzaa. Matumizi ya maji yanatakiwa yaangiliwe vizuri ili kuhakikisha kuwa maji hayazidi wala kupungua kwani maji mengi husababisha mizizi kuoza, ni chanzo cha magonjwa na mmea kudumaa. (Kangetakilimo)

UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA KABICHI
kabichi hupendelea udongo unaopitisha maji Kwa urahisi na 
wenye rutuba ya kutosha na hivyo hupenda Udongo 
uwe umetifuliwa vya kutosha au matuta kuruhusu mizizi kushika vema

AINA ZA UDONGO

Kuna aina kuu tatu za udongo,

• Kichanga (Sand soil) –

Una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.

• Tifutifu (Loam soil) –

 Unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.

• Mfinyanzi (Clay soil) –

 Unahifadhi maji mengi zaidi, Bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.

Vipimo vinavyoonyesha hali ya rutuba ya udongo ni:

 • Tindikali ya udongo

 • Kiasi cha mboji

 • Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa. Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)

PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).

AINA YA UDONGO UNAOFAA KWA ZAO LA KABICHI

Kabichi hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji. Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia halitaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH kiwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0 (kangetakilimo)

AINA ZA KABECHI

Early Jersey Wakefield  
Umbo lilochongoka kidogo, Hufunga vizuri,  Uzito ni kati ya kilo 1.5 hadi 2.0,Hukomaa mapema siku 90 – 100 tangu kupandikiza. ·

 Copenhagen Market:                                                                                             

  Vichwa vya mviringo na hupasuka kirahisi.Hukomaa mapema, siku 90 – 100 tangu kupandikiza ·

 PrizeDrumhead:      
  Vichwa vikubwa (kilo 2- 2.5), Vichwa ni bapa, huchelewa kukomaa (siku 110 – 120) –Huvumulia hali ya jua kali, Pia vichwa hupasuka. 

 Oxheart:       
  Vichwa vidogo huchongoka Kama moyo, Hupendwa Sana na walaji, LadhaYake ni tamu, hukomaa mapema, Hazina tabia ya kupasuka. 

 Glory of Enkhuizen: -      
   Vichwa vya mviringo, Huvumilia hali ya jua kali,  Huchelewa kukomaa (siku 110 – 120) na Ina tabia ya kupasuka.

JINSI YA KUANDAA SHAMBA
Unaweza kutumia trecta, jembe la mkono, ng’ombe kutayarisha shamba, shamba litayarishwe wiki moja kabla ya kupandikiza miche Kwa kutifua ardhi hadi kufikia kiasi cha sentimita 20 au30. Lainisha udongo na tengeneza matuta. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo moja hadi mbili, Kwa eneo la mita mraba 10. Mbolea hii iwekwe katika kila shimo. Kiasi kinachotakiwa ni kilo moja au kopo moja la Tanbond kwa kila shimo. Hii ni sawa kuweka na tani 10 hadi 20 kwa hekta. Katika sehemu zenye upungufu wa madini ya fosiforasi mbolea aina ya N.P.K yenye uwiano wa 5:15:5 itumike. Kiasi kinachotakiwa ni kifuniko kimoja cha maji ya uhai chenye gramu 10 kwa kila shimo la mche.

JINSI YA KUANDAA MBEGU KWENYE KITALU

Kitalu ni sehemu maalumu iliyopangiliwa kwa ajili ya kutunzia miche michanga kabla ya kuipeleka shambani ama bustanini. Sio mimea yote inahitaji vitalu ila mimea mingi inahitaji vitalu. Mimea Kama KABICHI, na yenye kuhitaji matunzo au kuhudumiwa kwa karibu wakati ikiwa michanga inashauriwa ipandwe kwanza kwenye kitalu hadi itakapopata miche inayotakiwa kisha kupandikizwa bustanini au shambani. Weka udongo debe mbili, mbolea debe moja na makapi ya mpunga ama mchanga debe moja (2:1:1).

Changanya vizuri kwa kutumia koleo na utandaze huo mchanganyiko kwa kutumiaa reki. Panda au sia mbegu bora ambazo zimekomaa na kukauka vizuri, ambazo hazijashambuliwa na magonjwa au wadudu na zenye uwezo wa kuota vizuri zikipandwa. Kama unahitaji kununua mbegu inashauriwa kununua

mbegu kutoka kwa mawakala wanaoaminika. Unaweza kupanda kwa mstari ama kwa kusia. Miche ikiwa tayari ikapandwe bustanini wakati wa jioni na imwagiliwe vizuri. Bustani iwe imeandaliwa kabla ya siku ya kuhamisha miche. Gramu 200 hadi 300 za mbegu zinatosha kupandikiza katika eneo la hekta moja. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe sentimeta 10 hadi 15 na kina kiwe sentimita 1.5. Baada ya kusia mbegu fukia na tandaza nyasi kavu na kisha mwagilia maji.

Endelea kumwagilia kitalu kila siku, asubuhi na jioni, hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku ya 5 hadi 10.Udongo kwenye kitalu unatakiwa uwe unaweza kupitisha maji vizuri. Tayarisha kitalu chako kwa kuchimba au kulima udongo angalau 30 sm kwenda chini, ondoa mabaki yoyote ya mimea na mizizi na vunja mabonge yote ya udongo kisha changanya samadi iliyooza vizuri au mboji iliyoiva vizuri. Sawazisha vizuri na reki hadi udongo uwe vizuri.

Pima upana na urefu wa kitalu ambao utakuwezesha kufikia kila pembe ya kitalu kwa urahisi bila kukanyaga ndani ya kitalu. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kuleta magonjwa kwenye kitalu na itarahisisha kungoa magugu pamoja na kuhamisha miche kwenda shambani.

Kama unasia mbegu katika mistari hakikisha kuwa mistari ipo katika umbali  Baada ya kusia mbegu funikia na udongo kidogo kutegemea na ukubwa wa mbegu. Siku moja kabla ya kusia mbegu, mwagia kitalu maji hadi kilowe vizuri. Kwa siku zinazofuata inashauriwa kumwagilia maji kidogo kidogo hadi pale zitaka

 SIFA ZA SEHEMU NZURI YA KUTENGENEZA KITALU

 1. Karibu na chanzo cha maji au bomba.

 2.  Sio mbali na shambani/bustanini.

 3.  Mbali na wanyama ama kuwe na uzio.

 4.  Pasiwe na upepo mkali

 5.  Iwe na kivuli.

 6.  Iwe karibu na njia kurahisisha usafirishaji pindi ikibidi.

MATUNZO YA KITALU

Baada ya kusia mbegu hakikisha kitalu hakipati jua la moja kwa moja na mvua kubwa. Weka matandazo ya majani ili kusaidia udongo kuhifadhi unyevunyevu na kuweza kuzuia mwangaza wa jua wa moja kwa moja.

Angalizo:

Ondoa matandazo mara tu mbegu zitakapochipua

 1. Ruhusu kivuli kidogo kwenye miche na usiweke kivuli kikubwa sana kwani kitaifaya miche isikue

 2. Baada ya kuchipua mwagilia maji taratibu kwa kutumia bomba au chupa yenye vitundu vidogo dogo. Hakikisha maji hayazidi kwenye kitalu kwani yanaweza kusababisha ugonjwa na miche kuharibika.

 3. Hakikisha kitalu ni kisafi wakati wote. Ondoa magugu yoyote yatakayojitokeza.

 4.  Punguzia miche kama imejazana sana ili kuipa nafasi ya kukua vizuri.

 5.  Kagua kitalu mara kwa mara kuangalia kama kuna uvamizi wowote wa wadudu waharibifu au mlipuko wa ugonjwa.

 6. Baada ya miche yako kufikia muda wa kupandikiza inashauriwa kuchagua miche yenye afya nzuri ambayo haijaathirika na wadudu wala kuwa na dalili yoyote ya ugonjwa.

Mwagilia maji kwenye kitalu usiku mmoja kabla ya siku ya kung’oa ili kurahisiha ung’oaji na kuzuia uwezekano wa mizizi kuharibika. Hakikisha miche iliyong’olewa haipati jua la moja kwa moja au hewa yenye joto. Inashauriwa kuiweka kwenye trei au kikapu na kuifunika na majani au nguo mbichi wakati inapelekwa shambani au bustanini.

NAMNA YA KUPANDIKIZA MICHE KWENYE SHAMBANI/BUSTANINI

 1. Panga kupandikiza miche shambani au bustanini siku ambayo jua siyo kali sana au wakati wa jioni wakati jua linakaribia kuzama.

 2.  Manyunyu ya mvua ni muhimu na husaidia sana wakati wa kupandikiza.

 3. Shindilia udongo vizuri kuzunguka mizizi ya mche kwa kutumia vidole vyako ili kuufanya mche ujishike vizuri kwenye udongo.

 4. Hakikisha unaweka nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea na mstari hadi mstari ili kuacha nafasi ya mizizi kutanukia na majani kuchanulia hapo baadaye.

 5. Kama hamna mvua wakati wa kupandikiza inashauriwa kumwagilia hata kama mimea haionyeshi dalili za kukauka.

 6. Ikinge mimea iliyopandikizwa na jua la moja kwa moja hadi wakati ambapo itaonyesha kuwa imeshika kwenye udongo, inaweza kukua yenyewe na kuhimili mwanga wa jua.

FAIDA ZA KITALU CHA MICHE KWA MKULIMA

 1. Kuchagua miche iliyo na afya nzuri.

 2. Kuthibiti magugu shambani kabla hajahamishia miche shambani.

 3. Kupata miche ya kupanda muda wowote atakao.

 4.  Ni rahisi kuthibiti vijidudu viharibifu na magonjwa kwenye kitalu kuliko shambani ama bustanini. Hii ni kwa sababu kitalu kinakua na miche mingi na

KUHAMISHA MICHE YA KATIKA KITALU

Miche huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki 3 hadi 5. Wakati huu huwa na urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (sawa na urefu wa kalamu ya risasi).Mwezi mmoja kabla kupanda miche, rutubisha udongo kwa kuweka mbolea za asili zilizooza vizuri. Mbolea hizi ni kama samadi, mbolea vunde na mbolea ya kuku.

Weka kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na kuweka ndoo moja hadi mbili zenye ujazo wa lita 20 katika eneo la mita mraba moja. Mbolea ya mchanganyiko aina ya N.P.K yenye uwiano wa 20:10:10 huwekwa kwenye shimo wakati wa kupandikiza mche. Kiasi kinachohitajika ni gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko mpaka kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa kila shimo.Upandaji wa Kabichi hufanyika kwa kupandikiza miche ambayo ipo tayari kwa kupandwa shambani, miche huwa tayari kupandwa baada ya wiki 3 – 5 tangu kusia kwa mbegu. Miche huwa na urefu wa sentimita 15 – 20. Ng’oa miche kwa uangalifu na pandikiza kama ilivyokuwa kitaluni na hakikisha mizizi haipindi wakati wa kupandikiza. Nafasi ya kupandikiza: Hutegemea aina ya kabichi – zenye vichwa vikubwa (Drumhead) ni sentimita 60 kutoka mche hadi mche na sentimita 75 toka mstari hadi mstari. – Zenye vichwa vidogo (Oxheart) ni sentimita 40 – 50 kutoka mche hadi mche na sentimita 60 toka mstari hadi mstari. – Umbali toka tuta moja na jingine ni sentimita 60. – Muda mzuri wa kuotesha ni asubuhi au jioni – Baada ya kupandikiza weka matandazo kama vile nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kuota kwa urahisi.

MBOLEA

Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea

Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:

1. Mbolea za asili (organic fertilizers)

2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile: 

i. Mbolea vunde:

 Inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.

ii.Samadi:

 kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.

iii.Mbolea za kijani:

Hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.

iv Majivu:

ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.

v.Matandazo (mulch):

Ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.

Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)

Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

Mbolea Za Kupandia

Mbolea maarufu za kupandia katika soko la Tanzania ni: TSP, DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao. Lakini zile ambazo zimechaguliwa kwenye mradi wa ‘Kukuza matumizi ya Minjingu Phosphate’ ni DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao.

  1. Diammonium Phosphate (DAP)

Ina virutubisho viwili - naitrojeni ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 18, na fosfati (P2O5) ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 46. Inapatikana katika hali ya chengachenga (granules).

  2. Minjingu Phosphate

Ina kiwango cha fosfati (P2O5) asilimia 29 na inatumika zaidi kwa kutoa kirutubisho hiki. Lakini inaongeza vilevile kirutubisho cha chokaa (calcium) ambacho kipo kwa kiwango cha asilimia 40. Chokaa inasaidia vilevile kukabili tindikali (acidity) ya udongo.

  3. Minjingu Mazao

Hii ni mbolea mpya inayotokana na Minjingu Phosphate lakini imeongezwa virutubisho vingine vitano ambavyo ni naitrojeni (10%), salfa (5%), zinki (0.5%), shaba (0.5%), boroni (0.1%), pamoja na chokaa (25% CaO) na magnesium (1.5% MgO). Virutubisho vilivyoongezwa hususani naitrojeni na salfa ni vile ambavyo vinakosekana katika aina nyingi za udongo.Zinki, Shaba na boroni vimeongezwa kwa tahadhari kwa sababu vinaonyesha dalili za upungufu katika baadhi ya maeneo. Minjingu Mazao iko katika hali ya chengachenga.

NAMNA YA KUCHAGUA MBOLEA YA KUPANDIA

Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao zinahitaji hali maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.Kwa mfano hali ya tindikali ya udongo inabidi iwe chini ya 6.2 ili mbolea za Minjingu ziyeyuke kwa kiwango cha kutosha. Kwa udongo wenye tindikali zaidi ya 6.2, tumia DAP wakati wa kupanda. Ikiwa kuna upungufu wa potashi, tumia mbolea zinazorejesha madini hayo.

Tumia mboji pamoja na mbolea za viwandani ili kuongeza mazao. Mboji huwa haibebwi na mvua na faida yake hudumu kwa muda mrefu. Mboji husaidia udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Zinapowekwa kwenye mashimo ya kupandia mbegu ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu (kutenganisha mbolea na mbegu).

1. Upungufu Wa Naitrojeni (Nitrogen)

Kwa ujumla mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo, na mwishowe hutoa mazao kidogo. Kama upungufu ni mkubwa sana mmea unaweza usitoe mazao. Kupungua Kwa kasi ya ukuaji wa mmea - ambayo husababisha mmea kudumaa. Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka taratibu kuelekea kwenye njano. Upungufu ukiwa mkubwa Sana, majani hugeuka rangi ya njano kutoka pembeni. Majani yaliyokomaa ndio huanza kugeuka.Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye naitrojeni ya kutosha.

2. Upungufu Wa Fosfati (Phosphorus)

Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa membamba. Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau. Rangi hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenye mashina na baadaye husambaa kwenye jani lote. Rangi inaonekana vizuri zaidi upande wa chini wa jani. Majani ya mwanzo hukauka mapema na mizizi haikui vizuri kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye fosfati ya kutosha.

3. Upungufu Wa Potashi (Potassium)

Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea kudumaa.Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis) kwenye mazao mengi, mazao mengine ya nafaka na miti ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na kukauka kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye Ncha.}UYR$%Y#@ u nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated). Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.


JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI WA KUPANDA KABICHI

Mbolea hizi ni kama samadi, mbolea vunde na mbolea ya kuku.Weka kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na kuweka ndoo moja hadi mbili zenye ujazo wa lita 20 katika eneo la mita mraba moja. Mbolea ya mchanganyiko aina ya N.P.K yenye uwiano wa 20:10:10 huwekwa kwenye shimo wakati wa kupandikiza mche. Kiasi kinachohitajika ni gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko mpaka kijiko kimoja kidogo cha chai au kifuniko cha soda) kwa kila shimo.PINGA SIMU +255717274387

JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI WA KUKUZIA KABICHI

Mbolea ya kukuzia aina ya CAN au S/A, YARAMILA NITRABO huwekwa wiki ya 4 hadi 6 baada ya mimea yako kutoka kwenye kitalu. Weka kiasi cha kizibo kimoja cha soda kuzungukia kila mche. Mbolea iwekwe katika umbali wa sentimita 10 kutoka kwenye shina. Hakikisha mbolea haugusi mche.

WADUDU

ü  Viwavi wa Kabichi (Diamond Backmoth)
Viwavi hawa huwa na rangi ya kijani kibichi na alama ya mstari wa kung’aa mgongoni, Nondo hutaga mayai chini yajani na baada ya kuanguliwa viwavi hula sehemu ya chini yajani na kuacha ngozi nyembamba mfano wa dirisha la kioo. Ni muhimu kuuwa viwavi kwa sababu ndiyo wanaoleta madhara makubwa.
Wadudu hawa wanaweza kuzuiwa kwa kunyunyuzia moja ya viuadudu  zenye kiambata cha:- Alpha-cypermethrin 10EC (systemic) lambda-cyhalothrin 5 SC au 100CS (Contact)Indoxacarb 14.5 EC au 150 EC/SL    (Contact),Lufenuron 500 EC (Contact),Deltamethrin 2.5 EC (Contact),Profenofos 500 EC au 720 EC (Cont

ü Inzi wa Kabichi (Cabbage Sawfly)
Mashambulizi hufanywa na kiluwiluwi mwenye rangi ya kijani kibichi au bluu. Hula majani yote ya kabichi na kubakisha vena au vishipa vya majani.
Inzi wa kabichi wanaweza kuzuiwa kwa kutumia viuadudu venye kiambata cha Acetamiprid + Lambda-cyhalothrin 60EC (Syatemic + contact)Imidacloprid + Emamectin benzoate 175SC/WDG (Systemic + contact)

ü  Sota (Cutworms)
Hawa ni funza wakubwa wenye rangi ya kijivu. Hupendelea kujichimbia katika udongo wakati wa mchana na kukata miche michanga karibu na usawa wa ardhi wakati wa usiku.
Zuia wadudu hawa kwa kutumia majivu au kiuadudu chenye kiambata cha Profenofos 500 EC au 720 EC (Contact) mara baada ya kupanda. Kama mche utakatwa, mtoe mdudu huyu kwa kumfukua na kumuua. Kisha pandikiza mche mwingine.

ü  Vidukari au Wadudu Mafuta (Cabbage Aphids)
Wadudu hawa ni wadogo sana wenye rangi ya kijani, nyeusi au khaki. Baadhi yao wana mabawa na wengine hawana. Hufyonza utomvu wa mimea na husababisha majani kubadilika rangi na kuwa meupe au njano iliyopauka. Mmea hudumaa na hatimaye hukauka.Wazuie wadudu hawa kwa kunyunyizia mojawapo ya viuadudu vifuatazo:- Acetamiprid 200 SC (Systemic) Cypermethrin+Imidacloprid 344 SE (Contact + systemic)

ü  Minyoo Fundo (Root knot Nematodes)
Hawa ni wadudu wadogo wanaoishi ardhini na ambao hawaonekani kirahisi kwa macho. Hushambulia mizizi na kusababisha kabichi kudhoofu na hushindwa kufunga vizuri. Mimea iliyoshambuliwa mizizi yake huwa na nundunundu.Wadudu hawa wanaweza kuzuiwa kwa kuzingatia yafuatayo:-

 • Utumiaji wa mbolea za asili kila msimu hupunguza kuzaliana kwa wadudu hawa.

 • Usipande kabichi mfululizo kwenye sehemu ile ile wala jamii yake kama vile kabichi ya kichina na kolifulawa, ila badilisha kwa kupanda mazao mengine kama vile mahindi, karoti, radishi na vitunguu.

 •  Ondoa masalia yote shambani ambayo yanaweza kueneza wadudu hawa na yachome moto.

 • pia utaweza tumia viuaminyoo

ü  African Mole Cricket
Hawa ni aina ya panzi ambao hujificha kwenye nyufa za udongo mchana. Hujitokezajuu usiku kwa kuchimba udongo kutumia miguuyambele. Wadudu, hawa huharibu mizizi na hula majani ya miche michanga.Zuia wadudu hawa kwa kutumia dawa ya Carbaryl. Changanya gramu 50 (vijiko vitano vikubwa vya chakula) vya dawa pamoja na kilo moja ya mchele, mtama au pumba za mahindi au ngano. Ongeza maji kidogo kwenye mchanganyiko huo na kisha mwaga kwenye njia wanazopita wadudu hawa.

 

MAGONJWA:

· Kuoza Shingo (Bacterial Softrot):

Ugonjwa huu husababishwa na vij idudu vya bakteria ambavyo viko kwenye udongo. Hushambulia kabichi na kuzifanya zibadilike rangi, kuoza na kutoa harufu mbaya. Vijidudu vidogo vidogo pia huonekana kwenye sehemu iliyooza.

Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-

 1. Epuka kujeruhi kabichi wakati wa kuvuna

 2. Vuna kabichi wakati hakuna mvua.

 3. Usilundike kabichi kwa wingi na kwa muda mrefu.

 4.  Hifadhi kwenye sehemu yenye ubaridi na yenye kuingiza hewa ya kutosha

 5. Ng'oa masalia, choma moto na lima shamba mara moja baada ya kuvuna.

 6. -Badilisha mazao.

· Uozo Mweusi (Blackrot).

Huu pia ni ugonjwa unaosababishwa na vijidudu vya backteria na hushambulia sana kabichi. Dalili kubwa za ugonjwa huu ni majani kugeuka rangi na kuwa ya njano na baadae kikahawia. Majani huanza kunyauka toka kwenye kingo zake na kuacha alama ya "V". Kingo zinakuwa na rangi nyeusi isiyokolea. Baadaye majani yaliyoshambuliwa hudhoofika na kupukutika. Kama ukikata jani au shina, mviringo mweusi huonekana kwenye vena. Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kuzingatia yafuatayo:-

 • Badilisha mazao kwa muda wa miaka miwili usipande kabichi najamii yake.

 • Panda kabichi kwenye sehemu ambayo haituamishi maji.

 • Kitalu na mazingira yawe safl daima.

 • Punguza miche ili kupunguza msongamano.

 • Ondoa masalia yote ya kabichi shambani baada ya kuvuna na yachome moto.

 • -Panda mbegu zilizothibitishwa na wataalamu.

​Kuoza Shina (Black leg).

Ugonjwa huu chanzo chake ni ukungu. Dalili kubwa za ugonjwa huu ni kuwepo kwa madoa yaliyodidimia yenye rangi ya kikahawia kwenye shina karibu na usawa wa ardhi, ikifuatiwa na kuvimba kwa shina. Baadaye uyoga mweusi huonekana kwenye uvimbe huo. Pia uozo wa rangi ya kikahawia huonekana ndani ya shina. Kwenye majani huonekana madoa meusi ya mviringo yaliyozungukwa na uyoga mweusi. Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-

 • Panda katika sehemu ambayo haituamishi maji.

 • Badilisha mazao; kwa muda wa miaka mitatu usipande zao la kabichi na jamii yake

 • Lima shamba mara baada ya kuvuna ili kuwezesha masalia ya mazao kuoza haraka kabla ya kupanda.

 • Ondoa kabichi zote zilizoshambuliwa shambani.

 • Tumia dawa za kuzuia magonjwa ya ukungu kama vile Ridomil.

· Uvimbe wu Mizizi (Clubroot):

Huu pia ni ugonjwa unaosababishwa na kuvu au ukungu. Hushambulia mizizi na dalili zake ni kudumaa kwa mmea na majam kukunjamana. Baadae mmea huoza.

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao.

· Madoajani Meusi (Black Leaf Spot):

Chanzo cha ugonjwa huu ni ukungu. Dalili zake m kuonekana kwa madoa madogo ya mviringo yenye rangi ya njano kwenye majani. Baadae madoa haya huwa makubwa na hugeuka kuwa

meusi.Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-

 1. Badilisha mazao

 2. Hakikisha shamba ni safi wakati wote.

 3. Ikibidi tumia dawa za ukungu kama vile Copperhydroxide (Kocide),Copper Oxychloride (Cupro).

· Ubwiri Vinyoya (Downy Mildew):

Huu ni ugonjwa wa ukungu ambao hupendelea sana hali ya unyevunyevu na baridi kali na huonekana zaidi kwenye kitalu. Dalili zake ni majani kuwa na mabaka ya mviringo yenye njano upande wa juu. Baadaye mabaka haya hubadilika na kuwa na rangi ya zambarau iliyochanganyika na nyeupe upande wa chini wa majani.

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kutumia njia zifuatazo:-

- Kilimo cha kubadilisha mazao

- Hakikisha udongo hautuamishi maji na kitalu ni kisafi wakati wote.

- Nyunyizia dawa za ukungu kama vile Zineb, Dithane M - 45, Copperhydroxide (Kocide) na Copper Oxychloride, Topsin -M na Ridomil.

· Kuoza Shina au Kinyawhi (Dampmg off or End Wire Stem):

Husababishwa na ukungu na hushambulia miche michanga. Miche iliyoshambuliwa huonyesha dalili za kunyauka, baadae huanguka na kukauka. Miche mikubwa huonyesha dalili za kudumaa. Sehemu ya shina iliyokaribu na ardhi hulainika na kuwa na rangi ya kikahawia.

Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa Kwa kutumia njia zifuatazo

- Punguza miche Kama imesongamana.

- Nyunyizia dawa za ukungu Kama vile Dithane M - 45, Ridomil, Thiophanate (Topsin - M).

KUVUNA                                                                                                                                   

 Kabichi hukomaa na huvunwa baada ya siku 60 mpaka 120 kutegemea aina ya mbegu iliyostawishwa tangu kupandikiza miche. Uvunaji hufanyika Kwa kukata shina sentimita mbili hadi tatu kutoka kwenye kichwa Kwa kutumia kisu. Ondoa majani ya nje na acha majani mawili au matatu ya kijani kwa ajili ya kuzuia kabichi zisikwaruzike na kuoza wakati wa kusafirisha. Punguza nusu ya urefu wa majani ya nje ili kurahisisha ufungaji. Kwa kawaida uvunaji hufanyika wakati wa asubuhi au jioni. Kiasi cha tani 40 au zaidi za kabichi kwa hekta hupatikana kama zao limetunza vizuri. Ondoa kabichi zilizooza au kuharibika wakati wa kuvuna. Kisha panga zilizobaki kufuata daraja Kama vile ndogo, za kati na kubwa. Kabichi ni zao linaloharibika kwa haraka, hivyo halina budi kutumika mapema iwezekanavyo baada ya kuvuna. Kabichi Kwa ajili ya kuuzwa zisafirishwe mara moja Kwa walaji. Kama usafiri ni mgumu, zihifadhiwe kwenye sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha. Wakati wa kusafirisha, ziwekwe kwenye matenga au visanduku vya

USHAURI:usilime kabda hujaa andaa soko usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo.

 

Habari? kangeta kilimo APP humsadia mkulima na mfugaji kutatua tatizo la magonjwa, Wadudu, magugu, masoko kwa urahisi kupitia simu yake ya mkononi PAKUA SASA PLAYSTORE???????? now

 

 

 

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.