Ni Nondo mwenye rangi ya njano na nyeusi anaeruka nyakati za usiku.Nondo huyu asili yake ni Amerika ya Kusini,Nondo huyu hushambulia mazao ya jamii ya nyanya (solanaceoue) kama:
§ Nyanya,
§ Bilinganya,
§ Pilipili hoho,
§ Nyanyachungu,
§ Viazi mviringo
§ Vitunguu.
BIOLOJIA, MZUNGUKO WA MAISHA NA TABIA YA KANTANGAZE
q Kantangaze huzaliana kwa haraka mara 10-12 kwa mwaka
q Mzunguko wa maisha huchukua siku 30-35 kutoka yai hadi nondo (mdudu kamili)
q Nondo wa Kantangaze huonekana muda wa usiku na hujificha katikati ya majani wakati wa mchana
q Nondo wa kike hutaga mayai hadi 260 yakiwa moja moja kwenye majani, shina na matunda machanga.
q Mayai huanguliwa kuwa funza siku 4-6 baada ya kutagwa
q Hatua ya buu hutokea katika udongo au kwenye michirizi iliyochimbwa kwenye majani na funza wa nondo wa kantangaze
q Hatua ya funza (Kiwavi) ndiyo iliyo hatari zaidi
UTAMBUZI WA NONDO WA KANTANGAZE
q Nondo wa kantangaze ana rangi ya kahawia iliyochanganyika na rangi ya brauni na ana urefu wa mililita 10
q Nondo wa kiume ana mchanganyiko wa rangi nyeusi kuliko nondo wa kike
q Mayai ya nondo wa kantangaze yana rangi ya njano
q Funza (Kiwavi) wa nondo wa kantangaze aliyeanguliwa toka kwenye yai ana rangi ya njano iliyopauka, akikua anabadilika kuwa na rangi ya njano iliyochanganyika na rangi ya kijani
q Funza aliyekua na kukomaa ana rangi ya zambarau upande wa nyuma ya mwili wa (funza) kiwavi na rangi nyeusi kwenye kichwa
q Mabuu (Pupae) yana rangi ya brauni inayong’aa (Light brown) na ina urefu wa milimita 6
Dalili zake mdudu kuwa shambani.
Tuta absoluta huwa anashambulia hatua zote za ukuaji wa nyanya kuanzia kwenye kitalu.hadi kweye tunda lenyewe .Mdudu huyu huyu anataka kufanana na leaf miner japo yeye anakula kila sehemu ya mmea tofauti na leaf miner anayeshambulia majani pekee.
Ni kuona majani yanakuwa kama yameungua ukitizama vyema utaona kuna uchafu wa rangi nyeusi waweza muona naye pia katika majani.hutaga mayai mengi sana ambayo huwa chini ya majani na huonekana kuwa na rangi nyeupe.
hatua yake ya ukuaji analeta madhara pindi akiwa funza anapokuwa mdudu kamili huwa kipepeo ambapo katika muda huo kazi kubwa ni kuzaliana.
Kwenye maeneo yenye joto kali sana ama baridi kali mdudu huyu hastahimili vyema sehemu hizo uzalianaji wake ni mdogo.
Wakati wa mvua hupunguza wingi wa mdudu huyu kwa kuwaua wale vipepeo na hivyo kupunguza kasi ya uzalianaji.
Kama nilivyokwisha sema anashambulia zaidi mimea jamii ya nyanya kuna taarifa toka Dodoma ameonekana kushambulia pia hoho.
NJIA ZA KUDHIBITI NONDO NA FUNZA WA KANTANGAZE
q Kagua shamba lako mara kwa mara ili uweze kutambua kama nondo, mayai, funza au viashiria au dalili za uharibifu katika zao la nyanya na uchukue hatua zinazostahili
q Kinga mazao kwa kutumia njia za kiutamaduni mfano, weka shamba katika hali ya usafi, tumia mbegu inayokinzana na nondo wa kantangaze kama zipo, kilimo cha kubadili mazao ambayo si jamii ya nyanya, panda mimea inayotoa harufu kati ya mstari na mstari au kupanda mimea inayozuia wadudu wasiingie shambani
q Ondoa masalia ya mimea ya nyanya baada ya kuvuna na choma moto
q Tumia mitego yenye mtego wa maji yenye harufu ya kipepeo jike, hivyo kuwa na uwezo wa kuvutia madume na mara yanapoingia yanakufa.
VIUADUDU (INSECTICIDES) VYENYE UWEZO WA KUDHIBITI NONDO NA FUNZA (VIWAVI) WA KANTANGAZE (Tuta absoluta)
ü Alpha-cypermethrin 10EC (systemic)
ü lambda-cyhalothrin 5 SC au 100CS (Contact)
ü Indoxacarb 14.5 EC au 150 EC/SL (Contact)
ü Chlorantraniliprole (Contact)
ü Lufenuron 500 EC (Contact)
ü Deltamethrin 2.5 EC (Contact)
ü Profenofos 500 EC au 720 EC (Contact)
ü Acetamiprid 200 SC (Systemic)
ü Profenofos+ Lambdacyhalothrin 315 EC/ULV (Contact)
ü Flubendiamide 480 SC (Systemic)
ü Chlorpyrifos (Contact) Emamectin Benzoate (Contact )
kumbuka
Chlorpyrifos kiambato amarifu hiki kinatumika kufukuza nondo wa kantangaze kutoka kwenye shamba, usinyunyiza moja kwa moja kiuadudu chenye kiambato cha Chlorpyrifos kwenye mazao, nyunyiza pembeni mwa shamba na kwenye njia kati ya mstari na mstari
Tumia Viuadudu vinavyotokana na mimea ya asili (Botanicals) Mfano, tumia Mwarobaini (uliotayarishwa kutokana na mbegu na majani ya Mwarobaini)
Tumia Bio-insecticides zilizosajiliwa Tanzania
Utaratibu wa kunyunyuzia viuadudu vinavyodhibiti nondo na kiwavi wa kantangazeza
v Pima kiwango sahihi cha kiuadudu kama ilivyoelekezwa kwenye kibandiko na kuchanganya kwenye ujazo wa maji uliopendekezwa
v Nyunyizia viuadudu mara tu unapoona dalili na viashiria vya kuwepo kwa nondo, mayai na viwavi katika shamba la nyanya. Rudia unyunyizaji wa viuadudu mara unapoona viashiria na dalili za kuwepo kwa kisumbufu katika shamba la nyanya.
v Nyunyiza asubuhi sana au muda wa jioni ambapo nondo wa kantangaze huonekana kwa urahisi au funza wanaweza onekana kwa urahisi kwenye majani na mashina
v Epuka kunyunyiza kiuadudu kukiwa na upepo mkali au mvua kwani huwa vinapunguza
uwezo wa sumu kufanya kazi iliyokusudiwa
v Ni vyema kuwa na utaratibu wa kunyunyizia mashamba yaliyo karibu na shamba lako ili kuepuka mashamba yasiyonyunyiziwa viuadudu kuwa mazalia ya nondo wa kantangaze
Angalizo: Viuatilifu ni sumu, unapovitumia ni vyema ukavaa vifaa kinga, kusoma kibandiko, kupima kiwango sahihi, muda wa kunyunyiza na muda wa kusubiri tangu uliponyunyiza kiuatilifu hadi kipindi cha kuvuna mazao. Pia usinyunyize kiuatilifu karibu na vynzo vya maji au sehemu ambazo kuna makazi ya nyuki