kilimo cha Dengu

kilimo cha Dengu

UTANGULIZI
Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma.Kwa Tanzania zao LA dengu hulimwa sana mikoa ya:


v Singida
v Dodoma
v Mwanza
v Iringa
v Manyara na
v Morogoro

HALI YA HEWA NA UDONGO
Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto kali na ukame sana huathiri mavuno yake,hupunguza wingi wa mavuno.Ni zao linalostahimili ukame,linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu.Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina tofauti tofauti wenye P.H 6-8.Udongo wenye asidi na base kidogo.

FAIDA YA ZAO LA DENGU

1.  Chakula chenye viini lishe vya protini,Mboga, bajia/vitafunwa

2.  Huongeza kipato na hupunguza umasikini

3.  Dengu ni zao jamii ya kunde hivo Hurutubisha udongo

4.  Huifadhi unyevu aridhini

5.  Kwa kuwa na uwezo wa kuvumilia maji kidogo Dengu Huongeza kipato na utajiri

UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba litayarishwe kwenye mvua za mwishoni baada ya kuvuna mpunga/mahindi Lima mara ya kwanza sm 15 (plough), rudia mara ya pili (harrow) ondoa miti,majani, mawe na mabonge ya udongo Lima kwa trekta, jembe la kukokotwa na ng’ombe/wanyama au jembe la mkono

MAANDALIZI YA MBEGU
Aina za mbegu na upatikanaji wake.

  • KUNA MBEGU YA AWALI,
  • MSINGI NA KUAZIMIWA(QDS)

Mbegu za dengu hazihitaji mvua nyingi kwenye kuotesha na kukuza Unyevu uliopo shambani baada ya kuvuna mazao mengine unatosha Husitawi vizuri kwenye mbuga ambapo maji hayatuami

AINA ZA DENGU
Aina za mbegu zilizothibitiswa na kufanyiwa utafiti Tanzania ni:
∙ MWANZA 1
Ni aina ya Desi rangi yake ni kahawia maua yake pia ni kahawia Mavuno ni mpaka 950kg/hekta ama ekari 2.5 Huchukua siku 83 kuanzia kupanda hadi kuvuna
∙ UKIRIGURUU 1
Ni aina ya Desi rangi ya mbegu ni kahawia, maua zambarau Kukomaa Kwa siku 93 Mavuno kilo 1000 kg/hekta/2.5 ekari
∙ MWAMZA 2 AINA YA KABULI
Mbegu za rangi ya maziwa, maua meupe
Mavuno 1000 – 1500kg/hekta/2.5 ekari Hukomaa siku 90
∙ MANGAZA AINA YA KABULI
Kukomaa siku 87 Mavuno mpaka kg 1000 kwa hekta/ekari 2.5

UPANDAJI WA MBEGU SHAMBANI
Mbegu zenye matawi kidogo:Msitari hadi msitari ni sentimeta 30 na shimo hadi shimo sentimeta 10 Mbegu zenye matawi mengi Msitari hadi msitari ni sentimeta 40 na shimo hadi shimo sentimeta 20 Panda mbegu 2 kwa kila shimo Baada ya wiki 6 kulingana na majani shambani, palilia Palizi hupunguza ushindani wa chakula, mwanga na mazalia ya wadudu

KUDHIBITI VISUMBUFU VYA MIMEA SHAMBANI
WADUDU WAHARIBIFU:
Funza Wenye tabia ya kufyonza kwenye majani, matawi, mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changa kama vitunda. Funza Wenye tabia ya kukata mashina na kuangusha mimea michanga na wengine hutafuna majani na maua.Funza wanaotoboa matunda/vitumba Chawa weusi au wa kijani (aphids) chini ya majani au kwenye shina:°Tumia viua tilifu au viua dudu pindi unapoona mashambulizi shambani°
Funza wanaotoboa vitumba: °Nyunyizia viua tilifu au viua dudu pindi vitumba vya maua vinapoanza kufunga, rudia mara ya pili baada ya siku 10 -14 mara ya 3 itategemea wadudu shambani°

viuadudu vinazopendekezwa;
LAMDA CYHALOTHRIN MF karate:~ changanya cc 40 kwenye lita 15 za maji
changanya cc 40 kwenye lita 1 ya ULVA
~Amerate: changanya cc 40 kwenza lita 15 za maji
~Profecron: changanya cc 40 kwenye lita 15 za maji.

MAGONJWA

1.  Mnyauko Fuzari Fusarium wilt (fusarium spp)

2.  Husababishwa na aina ya vimelea (fungus).

3.  vimelea huishi kwenye udongo na mbegu pia kwenye mabaki au tabaka za mimea zilizooza kwenye udongo.

ü DALILI
kulegea kwa majani na kuelekea chini
Mmea kunyauka na kufa kabisa Weusi katikati ya shina likipasuliwa
ü KUZUIA:
Kilimo mzunguko wa mazao Panda mbegu zinazostahimili ugonjwa Zingatia usafi wa shamba

CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU
Zipo chagamoto kadhaa katika kilimo cha dengu kama ifatavyo
1. Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazohujitokeza na kuharibu zao la dengu, yaani mvua za kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke ndio upande mbengu kama mbegu zimeharibiwa na mvua panda upya shamba lote.
2 Chagamoto ya Funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza tiba ya funza hao nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia
3 chagamoto ya wadudu wakati wakati mmea unatoa zao lenyeweWakati huu pia unapulizizia dawa kama wakijitokeza
Jambo la funza na wadudu hujitokeza mara chache sana hivyo ni vyema kuwana.tahadhali hiyo.
4 chagamoto ya panya Panya hujitokeza kwenye shamba wakati zao Linaanza kukomaa wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata hasara wakati dengu zilisitawi vyema Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu,dawa huchaganywa na mahidi nakusabaza pembezoni mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi na kuyala .Chagamoto nyingine ni za masika unaweza lima mwishoni sana kwenyemavuno ukakutana na mvua
5 chagamoto ya uhifadhi Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia nasiyo mifuko ya plastic Unashauriwa kutia dawa inaitwaAKTERIA mapema kabisa unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena Au unaweza hifadhi kwa mifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa.

UVUNAJI
Unashauriwa kuvuna mapema mimea inapokuwa imekomaa vizuri Epuka kuchelewa/ukichelewa utapata hasara ya wadudu, panya, ndege na kupasuka kwa vitumba

MAELEKEZO YA KUVUNA
Vuna mojamoja au ng’oa shina zima na sambaza kwenye eneo lililoandaliwa Kisha anika mbegu kwenye jua siku 2 kabla ya kupiga Hifadhi kwenye eneo lenye hewa nyingi Soko la dengu ni la uhakika sana kwa maana ya uhitaji wa dengu katika soko la ndani na nje Dengu ndiyo zao ambalo wakulima wa mikoa ya Singida na shinyanga,hulitegemea kwa kipato cha juu
Dengu gunia moja huuzwa mpaka sh
« 250,000 /= ,
« 200,000/=
« 180,000/=
« 150,000/=
Hizo ndiyo mbei za gunia la dengu Lakini bei hizo hutegemea msimu au mnunuzi na muuzaji . Pia gunia linakuwa na debe sita Ukitaka kuuza kwa kilo Misimu hutofautina wastani wa bei ni 1000 mpaka 1800 kwa kg 1 ya dengu.

ushauri maona wasiliana nasi 

  •  +255717274387/+255759417639
  •  Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

 

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.