Kilimo cha mahindi

kilimo cha mabogalishe (butternutsquash)

Mabogalise Hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.

 Mabogalishe  ni mojawapo ya jamii aina ya mbogamboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama matango,matikimaji na maskwash. Zao la mabogalishe(butternutsquash) ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine. 

Faida ni kubwa kwa mkulima, kwa kuwa zao hili huuzwa kwa kilo na ukubwa hutegemeana na matunzo shambani. Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa. Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha mabogalishe. 

 Asili ya bogalishe ni Amerika kaskazini, mabogalishe yamekuwa yakipandwa kwaajili ya biashara na kwaajili ya chakula. Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa maeneo mbalimbali duniani, Antarctika pekee ndiko maboga hayawezi kustawi. Mataifa yanayozalisha mabogalishe kwa wingi ni Marekani (USA), Canada, Mexico, India, and China.sourth Africa


Mabogalishe yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8. Pia udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60 °F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji yatakosekana

 KUTAARISHA SHAMBA NA UPANDAJI

 Baada ya kuchagua aina ya mbegu unayohitaji kupanda, inashauriwa kulima shamba na kuacha kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda miche yako ya butternutsquash (bogalishe).Hakikisha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika,

 udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini. Hakikisha kuwa shamba lako lina nafasi ya kutosha kwa kuwa Mabogalishe huitaji nafasi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kupata mwanga wa jua wa kutosha. Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 1cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 1 au 2 moja kwa moja katika kila shimo.

 Usipande katika kitalu kwasababu miche ya butternutsquash huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 60 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Kama utatumia njia ya fit nafasi kati ya mche na mche ni 50cm na stari na mstari ni 90sm

Zingatia kutokutumia mbegu za bogalishe uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa maboga yatakayozaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2) Kila shimo hakikisha umeweka mbegu 1 au 2 na uzipande kwa utaratibu Zikishaanza kutoa matunda hakikisha kila shina unaacha matunda matatu mengine kata ili kuruhusu ukuaji mzuri wa tunda kwani yakiwa mengi yatakuwa yanagawana chakula hivyo tunda kuwa dogo ambalo ukipeleka sokoni unapata pINA ZA MBEGU ZA BUTTERNUTSQUASH (MABOGALISHE)
Ni vizuri zaidi kununua mbegu za maboga zilizotayarishwa na zinazouzwa katika maduka ya pembejeo kuliko kutumia mbegu zile zinazopatikana baada ya kuvuna bogalishe na kisha kuondoa mbegu zilizo ndani na kukausha kisha kuotesha.kuna aina kuu mbili za mbegu za maboga lishe

1.    Kawaida (OPV variety)

2.    Chotara (Hybrid F1)

HALI YA HEWA
Kabla ya kupanda hakikisha kuwa udongo una joto la wastani wa nyuzi joto 70°C. Unaweza kupanda kwa kutumia jembe la mkono au reki. Fukia mbegu kwenye mashimo kwa kutumia udongo laini na shimo lisiwe na kina kirefu, liwe na wastani wa inchi 1, ili kutoa urahisi kwa mbegu kuota.

 Kwa kawaida maboga hupandwa kwa mstari mmoja kwenye tuta lenye mwinuko wa inchi 6 na upana wa futi 4. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimita 120 /60,80,90 .Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.

 Mabogalishe hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mabogalishe yatapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota Mvua: kwa upande wa mvua mabogalishe yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.

Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

 

 AINA ZA UDONGO

Kuna aina kuu tatu za udongo,

• Kichanga (Sand soil) –

una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.

• Tifutifu (Loam soil) –

 unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.

• Mfinyanzi (Clay soil) –

 unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.

 Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:

• Tindikali ya udongo

• Kiasi cha mboji

• Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa.

 Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)

PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).

 Mabogalishe hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.

 MBOLEA

Katika matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu, Lakini tumia mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo, ukihitaji kutumia mbolea za viwandani weka kiasi, sana, labda eneo hilo kama hakuna rutuba, mbolea ya DAP,CAN,NPK unaweza tumia.

MATANDAZO (MULCHES ),UPALILIAJI & UMWAGILAJI
Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingine kufunika ardhi.

Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako.

Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo. Palilia shamba nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba ili kuondoa wadudu. Shamba la mabogalishe linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga yaweze kustawi vizuri yasidumae.mwagia maji mara pindi unyevu unapotea shambani sio kila siku kwani mabonga yahaitaji maji ya kutosha

MAGONJWA YA MABOGALISHE

 Mangonjwa 

1)   Ubwiru chini

Huu ungonjwa husababishwa na fangasi (Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi,

 Dalili zake:

Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka  na madoadoa meus kwa mbali..

Tiba yake.

Tafuta kiuakuvu chenye  viambato...Metalaxyl na mancozeb nyunyiza kila baada ya siku 14

   2) Ubwiru juu

Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu Ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu).ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivu katika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani.

Tiba yake

Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza dawa za ukungu yenye kiambata cha ...Difenoconazole au Hexaconazole, na siku za upuliziaji itategemea muda wa kulima mabogalishe masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.ila tunashuri kila baada ya siku 14

  3) Ugonjwa wa virus

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi amabapo mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.na kukauka kabisa na matunda kuoza

 KUZUIA NA KINGA

 kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu.zui wadudu wanaofyonza katika shamba lako kwani wanaweza kueneza ugonjwa huu shambani kwako.

 Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa  sigara/tumbakukatika shamba la mabogalishe wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la mabogalishe.

 Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya maboga lishe.magonjwa ya virus huwa hayana tiba

    4) Mnyauko.

Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo na hata mikubwa huanzia aridhini ,husababisha miche kunyauka baada ya kula sehemu ya shina ugonjwa huu wakati mwingine huja kwenye mbegu.

Tiba yake.

kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu. katika shamba lako kwani wanaweza kueneza ugonjwa huu shambani kwako.

Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya maboga lishe.magonjwa ya mnyauko huwa hayana tiba

 

ITAENDELEA

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.