Makala

NZI WA MATUNDA (manyigu,madondola)

Kuna aina mbalimbali za inzi wa matunda wanaoshambuliwa mazao mbalimbali kama maembematikiti,ndizi,papai,machungwa,parachichi nk,  kangeta kilimo kitengo cha tafiti za visumbufu vya mazao

https://kangetakilimo.co.tz/pembejeo-za-kilimo

tumefanya tafiti mbali mbali za kuwasaidia wakulima nchini Tanzania kukabiliana na nzi wa matunda  kangeta kilimo tumefanya tafiti na kuona kuna aina 4 za Nzi wa matunda ambao husumbua mimea jamii ya matunda kwa kiwango kikuwa ambao ni

 

1) NZI WA MAEMBE (Ceratitis cosyra)

Nzi huyu hushambulia sana maembe na muenekano wake ana mwili Ana mabawa yenye rangi ya manjano na kwenye mzunguko wa kifuani  mwake  kuna madoa meusi:urefu wa mabawa yake ni  milimita nne hadi sita.sema inzi huyu hufanana sana na nzi wa mediteranean(ceratitis capitata) rangi na maumbile ya mabawa .Nzi huyu ameenea maeneo mengi ya Tanzania nzima na hushambulia sana maembe ,mapera ,manula nk

 

 2) NZI WA NATAL (Ceratitis rosa)

Nzi wa natal anasifa ya kuwa na mabawa  yenye mabaka ya kahawia na mabawa matatu sehemu ya nyuma ya kifua chake pia dume anamanyoa sehemu ya kati ya miguu yake.

Mzunguko wa maisha yake huanzia kwa nzi jike kutaga mayai kumi hadi ishirini ndani ya maembe na matunda mengine kwa wakati mmoja  hutanga mayai kwenye matunda yaliyokomaa na yaliyoiva mayai yake huanguliwa ndani ya siku nne baada ya kutagwa  funza hupitia hatua tatu na kuwa nzi kamili kwa muda wa siku kumi na mbili buu huchukua siku kumi na mbili hadi ishirini ndani ya udogo kabla ya kuwa nzi kamili nzi wa natal hushambulia matunda mengi kama papai,maembe,parachichi,mapera,kahawa

NZI wa natal anawezo mkubwa sana wa  kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa  hasa sehemu za joto na baridi anauwezo wa kuhimili sana mabadiliko makubwa ya hali ya joto kutoka sehemu za tropiki hadi sehemu zenye nyuzi joto chini ya sita za sentigredi

 

NZI WA MEDITERRANEAN(CERATITIS CAPITATA)

Nzi wa Mediterranean ameenea sana dunia nzima  inzi mpevu wa Mediterranean ana urefu wa  milimita tatu hadi tano  Nzi huyu ana anarangi ya manjano na kahawia kwenye sehemu za tumbo na miguuni mwao pia anamabaka kwenye mbawa zake na macho yake yana rangi nyekundu yaliyochanganyika  na zambarau nzi dume anavinyoleo viwili  vyenye virungu nchani  mbele ya kingo za macho yake

 

Nzi wa Mediterranean  hukamilisha mzunguko wa maisha yake ndani ya siku 30 na anauwezo wa kutaga mayai matatu hadi kumi ndani ya tunda  anauwezo wa kutanga mayai 20 kwa siku na mayai 870 katika maisha yake anashamulia matunda mengi sana kama maembe ingawa athari yake kwenye maembe sio kubwa sana kama kwnye kahawa ,machungwa,na ndizi

 

Kuna aina mbalimbali za inzi wa matunda wanaoshambuliwa mazao mbalimbali kama maembe,  kangeta kilimo kitengo cha tafiti za visumbufu vya mazao tumefanya tafiti mbali mbali za kuwasaidia wakulima nchini Tanzania kukabiliana na nzi wa matunda  kangeta kilimo tumefanya tafiti na kuona kuna   Nzi wa matunda ambao husumbua mimea jamii ya matunda kwa kiwango kikuwa

 

NZI MVAMIZI (BACTROCERA INVADENS)

 

Nzi mvamizi hufanana sana na nyingu rangi ya mwili  wake ni kahawia hadi nyeusi pembezoni  mwa mwili wake anarangi ya kahawia na nyeusi .pembezoni mwa kifua chake kuna mistari miwili ya rangi ya manjano mabawa yake yana mistari miwili yenye rangi nyeusi upande wa chini na juu tumbo lake lina rangi ya machungwa na kifuani mwake kuna alama ya 

 

Nzi huyu mvamizi hukamisha mzuko wa maisha yake ndani ya siku 22 hadi 30 anauwezo wa kutanga mayai 1000 katika mzunguko wa maisha yake.Nzi mvamishi ameeneoa sehemu kubwa mwa Tanzania na bara ya Africa .huyu ndie nzi anayeshambulia kwa kiwango kikubwa matunda aina nyingi sana kama jamii ya matango,maembe,machungwa, ndizi ,nyanya,kahawa,matunda ya porini,mapapi,parachichi,mapera huyu ndio nzi muharibufu kuliko nzi yeyote yule na husababisha harasa kwa kwa kiwango cha asimia 80.tunashauri wakulima kutumia juhudi ili kumzibiti huyu mdudu kwa kiwango kikubwa

 

MZUNGUKO WA MAISHA YAKE NA UHARIBIFU WA MBOGA NA MATUNDA

 Mzunguko wa maisha yake huanzia kwa jike kutanga mayai ndani matunda na mboga mboga kama maembe ,bamia,mapera nk kwa kutumia mwiba mkali mwishoni mwa tumbo lake uitwao msinzi akiwa na umri wa siku tano hadi wiki nane mayai huanguliwa ndani ya tunda na kuwa funza ambao hukua ndani ya tunda (Embe)huku wakila nyama ya tunda au mboga na kusababisha tunda kuoza na kudondoka chini kisha funza kutoka ndani ya tunda na kujichimbia ardhini kiasi cha sentimita mbili hadi tano na kuwa buu matunda yaliyoshambuliwa kwa kila tunda moja linaweza kuwa na wastani wa funza 60 hadi 100 kwa kila tunda.mzunguko kamila

 

1.    Yai huchukua siku mbili hadi tatu kuanguliwa kuwa funza

 

2.    Funza huchukua siku tatu hadi tano kuwa buu

 

3.    Buu huchukua siku  tisa hadi kumi na mbili  kuwa funa kamili

 

4.    Nzi mpevu huishi kwa wastani wa siku 40

 

  

 

NJIA TUNAZOPENDEKEZA KUZIBITI NZI AINA YA NZI WA 

Njia tunapendeka  kuzibiti  Nzi wa maembe aina ya Ceratittis cosyra ni kutumia njia za IPM kama kutumia mitego aina ya kangeta fruitfly aina ya augmentorium,pia unaweza kutumia njia ya kuweka chombo chenye protini kuweza kukamata madume pia udhibiti kibailogia matumizi ya viumbe maalum  Wadudu walangi(predators),vimelea(pathogens),manyingu(parasitoids) na maji moto

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.