Makala

Blossom End Rot (makovu meusi kwenye kitako cha tunda)

Hii ni changamoto linalotokea sana katika mashamba mengi ya bustani.Kitaalam huu sio ugongwa kabisa.Tatizo hili hutokana na upungufu wa Calcium na /au Umwagiliaji usiokuwa na mpangilio.

Huu sio ugonjwa wala wala madhara yatokanayo na uharibifu wa wadudu,ni ulemavu wa kiumbo unaotokana na upungufu wa Calcium katika tunda.
Chanzo kikuu cha tatizo hili ni umwagiliaji usiokuwa na mpangilio.Ukosefu wa maji ya kutosha husababisha upungufu au kiwango cha Calcium katika mmea. Ufyonzwaji wa Calcium kwenye mimea unauhusiano wa moja kwa moja na upatikanaji wa maji ya kutosha.

https://kangetakilimo.co.tz/pembejeo-za-kilimo

Nutrient Imbalance(Kutokuwepo Usawa wa Virutubisho).

Excess potash(Kuzidi kiwango cha Potassium kwenye udongo).
Inapotokea kiwango cha kirutubisho cha Potassium kimezidi au kipo kwa wingi kwenye udongo,hupunguza au kuzuia ufyonzwaji wa Calcium na hivyo kusababisha tatizo hilo.Kiwango cha Potassim kinaweza kuzidi hasa pale mtu anapotumia mbolea zenye potassium kwa kiwango kikubwa kuliko inavyoshauriwa kwa zao husika.(Recommended amount).

Jinsi ya kuzuia Tatizo.
Umwagiliaji.
Kitu cha msingi kabisa ni kuhakikisha udongo wako,au ardhi yako inakuwa na unyevu auhaikauki na kubaki kavu kabisa.Hakikisha kuna unyevu kwa ardhi yako japo kwa mbali na usiruhusu kabisa ardhi kuwa kavu .Ukame ni kitu kitu kingine kinaweza kusababisha tatizo hilo.

Matumizi ya Mbolea.
Kama umeshauliwa kutumia mbolea zenye potassium kwa jiri ya zao lako,hakikisha hutumii kiwango zaidi ya kile ulichoshauliwa.Kama umeshauliwa kutumia gram tano weka ,gram tano.Kama ni kumi tumia kumi.Potassium ikizidi,inakwenda kuzuia kabisa ufyonzwaji wa Calcium na hivyo kusababisha tatizo hilo.

KUZUIA TATIZO (Bloomsom End Rot).
Hakuna tiba ya tatizo hilo hilo kama tunda limeshaathirika.Mapema tu unapogundua tunda lina tatizo hilo,liondoe kutoka kwenye mmea husika.Ni vizuri na salama zaidi kulichimbia chini na kulizika kabisa.Hii husaidia nguvu nyingine kuelekea kwenye matunda ambayo hayajaathirika.

Weka mpangilio au ratiba nzuri ya Umwagiliaji kuwe na muda maalumu wa kumwagilia.Hii itasaidia kutatua tatizo katika njia mbalimbali.Kama matunda yataendelea kuathirika licha ya kuwa na ratiba nzuri ya kumwagilia,unahitaji kuangalia kiwango cha Calcium na Potassium na kufanya utaalamu wa kurekebisha kiwango kiwe sawa.

Kurekebisha kiwango cha Cacium katika mmea,unaweza kunyunyuza mbolea za majani zenye Calcium Nitrate angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa wki mbili na badilisha kwa kwa mlisho wa kawaida kwa kumwagilia mara moja kwa wiki maji yaliyochanganywa na Calcium Nitrate pia.

JINSI YA KUCHANGANYA MBOLEA KUDHIBITI TATIZO.

Calcium Nitrate Kama mbolea ya Majani.
Changanya kijiko kimojaa kisijae sana(1 level table spoon of Calcium Nitrate ) katika lita moja ya maji na mwagiia kwenye majani kama unavyofanya kwa dawa za kawaida na mbolea za majani(Wenyewe mnaita Booster).

Calcium Nitrate Kama mbolea ya kupiga kwenye Udongo.
Changanya kiwango kama kiichoelekezwa hapo juu, na kasha piga kwenye mashina kama mtu anamwagilia.

Pia mkulima anaweza kutumia Mbolea nyingine zinazoweza kutoa Calcium kwa haraka kama YARALIVA NITRABOR inayosambazwa na kampuni ya 

 

Hili tatizo linaitwa blossom end root. .
Tatizo huweza kusababishwa na mambo makuu mawili.
Kwanza kabisa ni utaratibu mbaya wa umwagiliaji wa zao la matikiti shambani. Yaani kubadilika badilika kwa ratiba ya umwagiliaji huweza kusababisha tatizo hili.
Pili, tatizo hili huweza kusababishwa na ukosefu au upungufu wa madini ya calcium kwenye udongo. Unapopanda zao lako la tikiti kwenye udongo ambao unakosa au kupungua kwa virutubishi hivi vya calcium kuna kuwa na uwezekano mkubwa wa matikiti hasa matunda ambayo bado ni machanga kukumbwa na tatizo la blossom end root au kuoza kitako.

Ili kuzuia tatizo hili , hakikisha kuwa unatenga siku maalum za umwagiliaji shambani kwako na hakikisha kuwa ratiba hiyo unaizingatia kwa kutoibadilisha badilisha,
Pili kwenye hatua za ukuaji wa mmea jitahidi kutumia mbolea zenye virutubishi vya calcium kwa wingi, yara nitrobor inaweza kuzuia tatizo hilo pamoja na mbolea zingine zenye calcium kwa wingi.

Vipimo vya mbolea hizi, tumia kiasi cha gm 5 au ufuniko mmoja wa chupa ya soda. Weka Kuzunguka shina la mmea wako au Pima sm 5 kutoka shina lilipo na uweke mbolea yako

www.kangetakilimo.co.tz

Kuhusu Kangetakilimo

Ni mtandao wa kilimo unaotumia malighafi za kilimo na masoko yaliyopo Tanzania ikiwa imelenga wakulima wadogo wa kati na wakubwa katikata kuwapatia njia bora za kilimo na technologia Kangetakilimo inawawezesha na kuwapa uwezo kwa kutumia technologia katika kilimo kwa mlengo wa kulima kibiashara.  .... Soma Zaidi

 

Download Kangeta Kilimo App

Please publish modules in offcanvas position.